Wakenya wameweza vipi kuwa na lipa namba mpaka kwa boda boda na wauza mboga?

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,480
Reaction score
38,367
Habarini wakuu? Kuna hili suala la cashless economy ambalo limekuwa likipigiwa chapuo mahala pengi duniani, ila kwa jirani zetu Kenya wameweza kulifanya kwa vitendo!
Hawa jamaa ukifika kwao kila mahali kuna lipa namba, kuanzia boda boda, wamachinga barabarani, wauza mboga mpaka daladala!

Yaani inafika mahala mtu unayelipa kwa cash ndo wanakushangaa, konda kabla ya kuondoa gari anawatangazia wanaolipa kwa "Lipa namba" wafanye hivyo na waoneshe message! Wengi kama sio wote wanalipa kwa simu, nilipodadisi zaidi nilikuja kugundua wale jamaa wana "zero fee" kwenye miamala ya kulipa!

Hili la zero fee naona ndo limewachagiza wengi kutotaka kuzunguka na cash kila mahali.

Sasa ukirudi hapa kwetu, fee kwenye lipa zinaenda kulingana na gharama ya kutoa hela kwa wakala! Nakumbuka makampuni ya simu yalidai watu walikuwa wakifanya ulaghai na kutoa hela kwenye lipa, ila kama kila mahali malipo yatafanyika kwa lipa watu watakuwa na haja gani ya kutoa hela wawe na cash? Cash wataipeleka wapi na kila mahali kuna lipa namba?

NB; Kule hata bando zao sio kama tunazokomoana hapa kwetu, tena haziishi kwa speed ! Mathalani 10k kule unapata 8gb wakati sisi 10k ni 4gb! Sasa sijui mchawi ni nani makampuni ya simu au CCM
 
nilipodadisi zaidi nilikuja kugundua wale jamaa wana "zero fee" kwenye miamala ya kulipa!
Hii ndio point kuu na muhimu, wengi wakija bongo hasa wakutoka Nairobi, Thika, Naivasha, Machakos na Kisii wanashangaa bado kuna cash na mistimu ya Fiber tunaweka plastic boxes
 
Hakuna kitu huwa kinanikera kutembea na cash mfukoni ,ndo maana chuma ulete ni wengi sababu mtu anatembea na rundo la pesa cash.
#ndo maana sipendi kuishi Tanzania.
 
Malipo ya lipa namba serikali itakuwa inaongeza kila mwezi kama kodi ya jengo tu kila mwaka wanaongeza wanadai gharama zinaongezeka nashindwa kuelewa gharama gani kwenye kodi ya majengo na sasa hv wamekuwa kiburi wanaongeza kimya kimya
 
Yaani wanafanya kama kukomoa vile!
 
Habarini wakuu? Kuna hili suala la cashless economy ambalo limekuwa likipigiwa chapuo mahala pengi duniani, ila kwa jirani zetu Kenya wameweza kulifanya kwa vitendo!
Hawa jamaa ukifika kwao kila mahali kuna lipa namba, kuanzia boda boda, wamachinga barabarani, wauza mboga mpaka daladala!

Yaani inafika mahala mtu unayelipa kwa cash ndo wanakushangaa, konda kabla ya kuondoa gari anawatangazia wanaolipa kwa "Lipa namba" wafanye hivyo na waoneshe message! Wengi kama sio wote wanalipa kwa simu, nilipodadisi zaidi nilikuja kugundua wale jamaa wana "zero fee" kwenye miamala ya kulipa!

Hili la zero fee naona ndo limewachagiza wengi kutotaka kuzunguka na cash kila mahali.

Sasa ukirudi hapa kwetu, fee kwenye lipa zinaenda kulingana na gharama ya kutoa hela kwa wakala! Nakumbuka makampuni ya simu yalidai watu walikuwa wakifanya ulaghai na kutoa hela kwenye lipa, ila kama kila mahali malipo yatafanyika kwa lipa watu watakuwa na haja gani ya kutoa hela wawe na cash? Cash wataipeleka wapi na kila mahali kuna lipa namba?

NB; Kule hata bando zao sio kama tunazokomoana hapa kwetu, tena haziishi kwa speed ! Mathalani 10k kule unapata 8gb wakati sisi 10k ni 4gb! Sasa sijui mchawi ni nani makampuni ya simu au CCM
Kwanza tukianza na mchawi hapo bila kupepesa macho ni CCM,
Sasa mwaka huu kuna sheria imepitishwa ambayo miamala yote inatakiwa kufanyika either kwa njia ya simu au bank....nafikiri kuanzia 1st January itakua ni kosa kisheria kupata huduma kwa malipo ya cash....lakini hadi sasa sheria ipo hai...imepitishwa kwenye hili Bunge haramu juzi.

Sema uchawi wa CCM unafanya tuwe na makato kwenye hizo transactions
 
Shule hatuna, kuna watanzania hawajui kutoa pesa kwa simu wala kutuma. anafika kwa wakala anampa simu wakala amtolee au amtumie pesa anaropoka na namba yake ya siri hapo, yani ni uzuzu mtupu!
inasikitishaa sana.
 
Hakuna kitu huwa kinanikera kutembea na cash mfukoni ,ndo maana chuma ulete ni wengi sababu mtu anatembea na rundo la pesa cash.
#ndo maana sipendi kuishi Tanzania.
Watu wanahangaika sana kutafuta chenji.,imagine boda kakubeba unashuka unampa elf 10 anaanza kutoa macho!
 
Back
Top Bottom