Sikuwa nataka kukuquote ila wakati mwingine inabidi. Mzee kama ungeingia darasa la uhasibu ungefahamu kwamba katika kurekodi mapato na matumizi, mapato yako ni matumizi ya mwajiri wako. Sasa GoK inapolipa wafanyikazi wake mishahara hio ni matumizi kwa GoK ila ni mapato kwa wafanyikazi. Kwa hivyo wafanyikazi watairekodi kama mapato na GoK itairekodi kama matumizi.
Tukija kwenye remittance, waajiri wa nchi za ulaya walioajiri Wakenya na kuwalipa mishahara watarekodi mishahara hizo kama expenses au matumizi ya kampuni zao. Wakenya wanaopokea mishara hizo watazirekodi kama mapato waliyopokea. Sasa Wakenya hao wanapotuma pesa hizo nyumbani Kenya, nchi hio ya Ulaya itarekodi pesa hio inayotumwa kama capital outflow na Kenya ambayo inapokea pesa hio itarekodi pesa hio kama capital inflow. Central Bank of Kenya ndio ina jukumu la kurekodi hizi pesa zinazoingia katika uchumi wa Kenya kutoka ulaya na huwa wanatoa ripoti kila mwezi.
Halafu nimesema remittance ni capital inflow, wewe utakuja kupinga na kusema kwamba remittance sio investment. Hii ina maana kwamba hujui tofauti kati ya capital na investment. Jifunze tofauti kati ya capital na investment ndio uje udebate na mimi. Capital is a broad term kushinda investment na inajumlisha investment na mambo mengi zaidi ya investment. Remittance ni capital kwa maana fedha ni capital. Pesa ni capital. Sasa wewe ukisema remittance sio capital inflow ina maana kwamba hujui kwamba pesa ni capital na pia hujui kwamba pesa inapoingia ndani ya nchi hio inaitwa capital inflow?
Mwisho kabisa, remittance inaleta foreign exchange earnings ya $3 billion kwa Kenya kila mwaka. Sasa wewe sio mjinga, wewe unajua umuhimu wa kuwa na foreign exchange reserve ya kutosha katika uchumi husika. Bila foreign exchange reserve ya kutosha nchi inakufa. Nchi ikikosa foreign exchange reserve itakosa dollars ya kununua madawa kutoka India kwa ajili ya mahospitali. Itakosa dollars ya kununua mafuta ya diesel na petrol kutoka nchi za Kiarabu. Itakosa dollars ya kununua fertilizer kutoka Russia. Najua bado utagandia point yako kwamba remittance haina umuhimu wowote katika uchumi wa Kenya. Hapa ni kama nimepoteza muda tu kuongea na jiwe ambalo halina masikio. Lengo langu ni kuelimisha watu wengine wataosoma hii message, sio wewe.
Geza Ulole