Woga, uvivu na ujinga ndio kila siku vinatufanya Watanzanzania kuwaogopa. Unaposema fursa za kazi walizoumbiwa Watanzania una hakika na hilo au ni hisia zako zimekutuma?
Wakenya waruhusiwe haraka sana kuja kufanya kazi na biashara, tutafaidika sana na uwepo wao ktk nyanja za elimu, afya na biashara. Fursa za kiuchumi na ajira zitaongezeka na sio kupungua kwa sababu wataleta mapinduzi ya kifkra na ki utendaji hivyo kuchochea ukuaji wa uzalisha na uchumi.
Kitu kimoja tu ni kuwa Wakenya (na wageni wengine wowote) wasipiwe fursa ya kununua na/au kumiliki ardhi. Jambo hilo liwe nje ya mada hiyo.
Mwisho lazima Watanzania tujifunze kuiga mambo mazuri na kukataa mabaya. Mfano vyama vyetu vya ushirika na hata nyingi ya SACCOs bado hazijaleta matokeo kama ambayo wenzetu Kenya wamekuwa wakifaidika. Sasa kwanini tusiige hata jambo dogo kama hilo? Kwa nini tunaona mabaya tu ilihali fursa ya mema ni kubwa zaidi???
Kwa heshima nyingi naomba Rais wetu Mh. John Magufuli ukubali fursa hiyo muhimu. Ikiwezekana ufute mara moja hilo zuio na tufanye kazi badala ya kushindana na kuwaona jirani zetu hao kama maadui.