Wewe tatizo una mawazo ya kizamani sana, pia inaonekana huna exposure ya dunia, unachokiamini wewe unataka kiwe kama kilivyo, na usichokiamini wewe basi hakifai, wapo wanaopenda hiyo natural skin kama wewe, lakini walio wengi wanapenda watu waliojipodoa na kubadilisha skin iwe a bit light, ndiyo sababu biashara hiyo imekuwa kwa kasi sana duniani, kuna wanaopenda natural hair, lakini wengi wanapenda nywele bandia, kwanini unapingana na dunia?
Nimesema mwananmke anajiremba ili avutie wanaume wa hali ya juu kimaisha, watu wenye hali nzuri wanapenda kuoa wanawake warembo, na urembo wa mwanamke unaongezwa na vipodozi, wachache kama wewe ndiyo wasiopenda vipodozi.
Kuhusu hizo taarifa za kina Flavian kupata pesa nyingi za matangazo, kwanza hazihusiani na mjadala wetu, mjadala ni kupendeza kwa mwanamke na kupendwa kwa wanawake kati ya wanaojichubua na wasiojichubua, sasa hayo ya kupata pesa nyingi yanakujaje hapa?, unadhani hao unaowataja kigezo cha kupata hizo pesa ni kutojichubua?, zaidi ya hayo yote usilete habari za udaku usizokua na ushahidi ili muradi tu ujaze server ya JF, lete ushahidi kuonyesha kwamba alilipwa $1.5m katika tangazo alilofanya.