Wakiambiwa wabuni vyanzo vya mapato wanafikiria kuongeza kodi?

Wakiambiwa wabuni vyanzo vya mapato wanafikiria kuongeza kodi?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Sasa ukiongeza kodi ndiyo umebuni nini? Kuna ubunifu gani hapo?

Badala ya kuumiza kichwa uchumi ukue ili uweze pata kodi ya kutosha wewe unaongeza kodi, ambayo nayo ni hatari kwa uchumi kukua, harafu unasema 'tumebuni' vyanzo vya mapato!

Tutafute njia za kutumia rasilimali zetu kukuza uchumi, huko ndiko akili yetu itumike na kuumia sana. Na si kutafuta njia za kufanya unyang'anyi daily.

Niccolo Machiaveli anasema kiongozi anatakiwa kuepuka sana kuwa mporaji. Anasema mtu anaweza sahau kifo cha baba yake lakini hawezi sahau akiporwa mali aliyoachiwa naye.

Anamaliza kwa kusema; uporaji hufanya kiongozi achukiwe. Na katika mambo ambayo kiongozi anatakiwa kujiepusha sana ni kuchukiwa na kudharauliwa.
 
Kulaumu kazi rahisi sana lakini kuja na wazo mbadala lenye mantiki ndipo mtihani ulipo.
Ndiyo maana wana wizara nzima yenye wasomi waliobobea. Wanaresource zote za kufanyia utafiti na ubunifu. Na kuna planning commision ya nchi(national think tank). Watu kama hao hatutegemei ubunifu wao uwe kuongeza kodi.
 
Wawekezaji wapya wa nje hawataki kuja kutokana na uzembe wetu wa kushughulikua COVID-19.
Viongozi wetu wabuni vyanzo vipya vya mapato bila kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu zaidi, mambo yakizidi kuwa magumu wataingia barabarani
Na mbaya zaidi kwa nchi za kidemokrasia ni kuwa matumizi huongezeka kila siku, kila siku serikali itahitaji fedha zaidi. Sasa kama solution ni kuongeza kodi kila siku, itafika sehemu haitawezekana
 
Ndiyo maana wana wizara nzima yenye wasomi waliobobea. Wanaresource zote za kufanyia utafiti na ubunifu. Na kuna planning commision ya nchi(national think tank). Watu kama hao hatutegemei ubunifu wao uwe kuongeza kodi.
Wanafanya mengi kulingana na dunia hii ya covid19 kumbuka lipo ongezeko la watu lakini rasilimali haziongezeki.

Tulipofikia kukaribia uchumi wa kati ngazi ya katikati ni jitihada zao, wanafanya mengi laki ni hatuyaoni tukiwa ni mabingwa wa malalamiko.
 
Hakuna cha maana. Serikali nayo inafanya kazi ya kijungu jiko. Inaokotaokota pesa ili siku ziende. Na huo uchumi wa kati wa chini bado ni umaskini mkubwa sana, nchi yetu bado ni moja ya nchi maskini duniani. Hakuna hatua ya maana tumepiga.
 
Kutajirika sio suala la siku moja au mbili ni mchakato wa miaka mingi.

Ukarabati wa bandari ujenzi viwanja vya ndege ndio njia za kuifungua nchi iweze kupaa kiuchumi.

Kuna tozo za anga ni mabilioni ya pesa yanayoingia hazina kila mwaka, kuna mapato mengi tu usidhani ni hizi za simu pekee.

Ni mtazamo wako lakini hakuna wa kukubadilisha.
 
Wanafanya mengi kulingana na dunia hii ya covid19 kumbuka lipo ongezeko la watu lakini rasilimali haziongezeki.

Tulipofikia kukaribia uchumi wa kati ngazi ya katikati ni jitihada zao, wanafanya mengi laki ni hatuyaoni tukiwa ni mabingwa wa malalamiko.

Ni mataifa machache sana yameendelea kwa kutegemea raslimali pekee, bali uzalishaji mali. Ndio maana unasikia porojo za kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi mpaka wazungu wanatuonea wivu, lakini hizo raslimali hazitutoi.
 
wenye mawazo sahihi mnawapora kura, mnalazimisha kutawala msio na uwezo mnasubiri mpewe mbinu ya kutawala.
Wenye mawazo sahihi kwa mtazamo wako ni wepesi sana kwa mtazamo wa walio wengi.

Kutawala ni suala pana na lenye kutazamwa kadri ya fikra za mtu binafsi.
 
Sasa ukiongeza kodi ndiyo umebuni nini? Kuna ubunifu gani hapo?

Badala ya kuumiza kichwa uchumi ukue ili uweze pata kodi ya kutosha wewe unaongeza kodi, ambayo nayo ni hatari kwa uchumi kukua, harafu unasema 'tumebuni' vyanzo vya mapato!
Tutafute njia za kutumia rasilimali zetu kukuza uchumi, huko ndiko akili yetu itumike na kuumia sana. Na
si kutafuta njia za kufanya unyang'anyi daily.

Niccolo Machiaveli anasema kiongozi anatakiwa kuepuka sana kuwa mporaji. Anasema mtu anaweza sahau kifo cha baba yake lakini hawezi sahau akiporwa mali aliyoachiwa naye. Anamaliza kwa kusema; uporaji hufanya kiongozi achukiwe. Na katika mambo ambayo kiongozi anatakiwa kujiepusha sana ni kuchukiwa na kudharauliwa.
We unaona kodi ya miamala si ubunifu? FAILED STATE kila mtu ni kambale, na maza alivyosoft watu wakibweka anaufyata.

Kodi za miamala ni miongoni mwa kodi laini mtu analipa bila kuumia kivile. Ni kama serikali ilivyofuta road licence za watu kujisweka kama magunia mmejipanga eti mnaenda kulipa TRA. Walivyoamua kuiweka iwe automatic kwenye kununua mafuta watu tunalipa bila hata kustuka.

Bottom line ni kwamba kila mtanzania lazima achangie maendeleo ya nchi yake, ni namna gani bora ya kufikia hapo ndio ubunifu huo unatakiwa.
 
Kutajirika sio suala la siku moja au mbili ni mchakato wa miaka mingi.

Ukarabati wa bandari ujenzi viwanja vya ndege ndio njia za kuifungua nchi iweze kupaa kiuchumi.

Kuna tozo za anga ni mabilioni ya pesa yanayoingia hazina kila mwaka, kuna mapato mengi tu usidhani ni hizi za simu pekee.

Ni mtazamo wako lakini hakuna wa kukubadilisha.
Hiyo ni kauli dhaifu, binadamu hatuishi milele. Kuna nchi zimetoka kwenye umaskini ndani ya 10years. Mtu anazaliwa na kufia kwenye umaskini halafu unasema maendeleo siyo ya siku moja.
 
Back
Top Bottom