Wakiambiwa wabuni vyanzo vya mapato wanafikiria kuongeza kodi?

Wakiambiwa wabuni vyanzo vya mapato wanafikiria kuongeza kodi?

Sasa ukiongeza kodi ndiyo umebuni nini? Kuna ubunifu gani hapo?

Badala ya kuumiza kichwa uchumi ukue ili uweze pata kodi ya kutosha wewe unaongeza kodi, ambayo nayo ni hatari kwa uchumi kukua, harafu unasema 'tumebuni' vyanzo vya mapato!

Tutafute njia za kutumia rasilimali zetu kukuza uchumi, huko ndiko akili yetu itumike na kuumia sana. Na si kutafuta njia za kufanya unyang'anyi daily.

Niccolo Machiaveli anasema kiongozi anatakiwa kuepuka sana kuwa mporaji. Anasema mtu anaweza sahau kifo cha baba yake lakini hawezi sahau akiporwa mali aliyoachiwa naye.

Anamaliza kwa kusema; uporaji hufanya kiongozi achukiwe. Na katika mambo ambayo kiongozi anatakiwa kujiepusha sana ni kuchukiwa na kudharauliwa.
Na hiyo tozo wanakwenda kufanyia maonyesho badala ya kufanyia miradi productive

 
We unaona kodi ya miamala si ubunifu? FAILED STATE kila mtu ni kambale, na maza alivyosoft watu wakibweka anaufyata.

Kodi za miamala ni miongoni mwa kodi laini mtu analipa bila kuumia kivile. Ni kama serikali ilivyofuta road licence za watu kujisweka kama magunia mmejipanga eti mnaenda kulipa TRA. Walivyoamua kuiweka iwe automatic kwenye kununua mafuta watu tunalipa bila hata kustuka.

Bottom line ni kwamba kila mtanzania lazima achangie maendeleo ya nchi yake, ni namna gani bora ya kufikia hapo ndio ubunifu huo unatakiwa.
Kodi kwenye miamala ilikuwepo kabla . Kilichofanyika ni uporaji tu wa hela za wanaotumia miamala! Hapa cha msingi Kila mtu aangalie urahisi wa maisha yake . Mimi kwa upande wangu nimeona Bora nitumie njia ya benki
 
Li nchi likuubwa ardhi tele,limezungukwa na maziwa na bahari cha kufanyia hawaoni wanategemea vikodi vya maskini wasiofika mil 30(wanaofanya miamala) aibu na ufukara mkubwa!!
 
Back
Top Bottom