Wakili: Akina nyundo wanaona hawajatendewa haki ndio maana wamekata rufaa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wakili Meshack Ngamando, anayewatetea warufani wanne waliohukumiwa kifungo cha maisha jela, amefafanua kuwa rufaa yao inayoendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma haitajumuisha ushahidi mpya. Badala yake, Ngamando amesema wao kama mawakili watetezi watajikita katika kueleza mapungufu yaliyopo kwenye kesi ya msingi.

Ngamando aliyasema hayo leo Juni 9, 2025, nje ya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki jijini Dodoma, kabla ya kuingia mahakamani kusikiliza rufaa hiyo. Rufaa hiyo inawahusu Clinton Damas maarufu kama Nyundo (askari wa JWTZ), Praygod Mushi (askari magereza), Nickson Jackson, na Amin Lema, ambao walihukumiwa kwa kosa la kumbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya. Hukumu hiyo iliambatana na faini ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja.
 
After all waliyoyafanya? Dammmm
 
Dada wa yombo dovya aliwahimili kikamilifu.
 
Back
Top Bottom