Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakili Boniface Mwabukusi ambaye ni mmoja wa mawakili wanaowawakilisha walalamikaji kwenye kesi ya kupinga mkataba wa bandari iliyofunguliwa mkoani Mbeya, ameitikia wito wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya baada ya kuitwa (kwa njia ya simu na maandishi) na polisi siku chache zilizopita.Haijajulikana bado kwamba Wakili Mwabukusi anayeongoza jopo la wenzake kuwatetea walalamikaji kwenye kesi hiyo anahojiwa kuhusu nini hasa.