Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Kwenye mpira wa miguu kuna mashuti yale yanayopigwa kutoka mita 18 wakati huo kipa anakuwa kasogea kidogo mbele ya goli hategemei kama shuti litapigwa sàsa uone jinsi anavyohangaika.
 
Hivi watu wasiojulikana wameshaisha au siku mwendo wa mahakamani!
 
Wapatikane watanganyika majasiri kama huyu, wawe wengi wa kutosha kabisa. Maneno mazito kwa sie waoga, ila yana uzito.
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Huyu ni mwanasheria, anajua sheria, anajua Katiba ya nchi halafu anazungumza maneno makali namna hii? Hii paragraph ya tano inasikitisha sana. Hivi huu ni uhuru wa kutoa maoni? Hebu tuwe na heshima, hekima na busara ktk masuala ya nchi. #Muungano hauvunjiki ng'oo.🙏🙏🙏
 
Huyu jamaa nimemkubali sana na napenda sana kumsikiliza. Huyu ni mmoja wa vijana aliowatabiria mwalimu J. K Nyerere kwamba anataka Tanzania iwe na vijana jasiri wenye kuhoji mamlak kwa facts bila uwoga wowote
 
Magu ndio alijenga SGR ili ichukue mzigo wa Rwanda. Na Kagame Rais wa Rwanda kafungua dry port ya kuweka mzigo unaokusanywa ili uweze kusafirishwa kuja huku Dar kupitia SGR.

Samia anaposema kazi iendelee huwa haeleweki anamaanisha nini, ni muendelezo wa biashara iliyoanza kufikiriwa kufanyika tangu miaka ya 2014-15. Hawa kina Mwabukusi wanapotosha lengo nzima la mradi wa muda mrefu kwa kutumia siasa za chuki, huyo mwanasheria kwa sasa kawekwa kiporo kwanza ili masuala mazito yaweze kufanyika.

Awe mwangalifu kwani anapigana na serikali isiyoonekana kwa macho yetu haya mawili.
Acha habari za vijiweni. Na vitisho vya kijinga. Eti kiporo!!
 
Tunawaomba sana asidhulike wakili msomi kwani huyu ndiye mboni yetu sisi watanganyika au vinginevyo mtaleta machafuko
Machafuko? toka barabarani halafu utajuwa maana ya machafuko, kwa kuwa bado imejificha humu na ID fake endeleeni tu ila siku mkijion vidume tokeni hadharani halafu ndio utajuwa kumbe kuna serikali.
 
Wapatikane watanganyika majasiri kama huyu, wawe wengi wa kutosha kabisa. Maneno mazito kwa sie waoga, ila yana uzito.
Mbona mko wengi humu na mnatukana kumbe majasiri hawafiki hata 20?
 
Hamna red line yoyote, Mama yenu hatafanya chochote anaogopa Wamarekani na vyombo vya usalama wanajua hawana mtetezi pale.
Sasa mnashindwa nini kutoka barabarani, tokeni halafu ndio utajuwa shughuli zetu, hakikisha umeaga kwenu vizuri.
 
Wakili Mwabukusi hapo amezidisha ukali wa maneno na matamshi yake, tena sana. Mpaka roho imenistuka dah!!!

Hata viongozi wa vyama vya upinzani kina Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Zitto Zuberi Kabwe, Yuda Iskarioti (Prof Lipumba) hawajawahi kutoa matamshi makali kiasi hicho!

Sisi wengine kila kukicha tunaitoa kasoro Serikali, Mawaziri na CCM kwa maamuzi wanayofanya, tokea enzi za mwendazake. Kila siku tunavurugana nao mitandaoni... Ila hatujawahi kuthubutu kufikia kutoa maneno makali na yenye ukakasi kiasi hicho!

Mungu iongoze Tanzania, Mungu Ilinde Tanzania. #TanzaGiza!
Yuko sawa kabisa. Sema Bongo tumekuwa na tabia za Uoga Uoga. Hata humu jukwaani tunaendelea Uoga.

CCM na serikali yake wameshindwa kujibu hoja za msingi. Waziri Mkuu yuko busy wanapotosha halafu anasingizia wengine kuwa wanapotosha.
 
wameyataka wenyewe. ameongea mambo yoote sahihi, na ukweli ni kwamba, hicho alichoongea ndicho kilichojaa kwenye mioyo ya Watanganyika. ila kwa mbali wanafanya unafiki kwasababu walijengewa hofu tangu enzi za nyerere, hadi leo, na kuiacha Tanganyika inapotea na zanzibar inaneemeka kutokana na Tanganyika.
 
Sijaelewa unatafuta namba ya majisiri au nini?
Tuwaone barabarani halfu tutajuwa kiwango chenu cha ujasiri. Fanyeni yote lakini mtu akitaka kutuletea uchafu katika nchi yetu hii ya amani atashughulikiwa hata family yake siku ya kukuaga watakukana kama wanakujuwa.
 
Back
Top Bottom