Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Ni kweli atakipata lkn hiyo ndio sauti halisi ya Mtanganyika huu ndio uharisia usio hasiwa na hakuna sauti yoyote Toka kwa mtu yeyote nje na ndani ya Tz itakayobadili hayo milele asanteni
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Nchi hii Ina waoga Sana ,kwani lazma amsifie tu ,freedom of speech ipo kikatiba ,amiri jeshi mkuu kitu gani ,yy ni mtu Kama wengineo ,rais na waziri mkuu waliambiwa na nani wapo above the law ,hivyo viti SI vya mama Yao ,eti waogopewe ,kifo ni siku Moja wabaki wakijua siku zao in the sun ni chache
 
Waoga ndio waliwao ,mawakili na wasomi wengi wanajua nchi inaongozwa vibaya mno ,huku nje machawa wanasifia Bure
Mama alizindua miradi mingi ambayo mwendazake hata na ubaya wake yy ndiye aliyeanzisha kisha sifa mna mpa mwingine .ukweli usemwe peupe
 
Ametumia lugha Kali sana ili ujumbe ufike na machungu yake ni machungu ya kitaifa na ndio sauti ya wananchi huu ni uharisia
 
Mungu yuko kazini!! Haya maneno, na huu ujasiri, na hizi hatua anazochukua inaonekana kabisa kuwa Mungu amempaka mafuta wakili Boniface Mwabukusi na kumtia nguvu ili kulinda utajiri na ,maslahi ya nchi yetu!! Nawaonya "watawala" msimwone Boniface kama Boniface!! Ni Mungu yuko kazini akimtumia Boniface!! Atakayejaribu kumshambulia kitakachompata asije kusema sikujua wala sikuambiwa!!
 
Mungu anaweza kumtumia yeyote aliye tayari!! Ni aibu kwa watu walio kwenye nafasi ya kulinda maslahi yetu lakini kwa WOGA au kwa kupewa "kitu kidogo" wameamua kufumba macho na kuziba masikio HASA WABUNGE. Ninyi mmekaa kimya na Mungu amejipatia mtu baki (yaani aliye nje ya serikali) aliye tayari kutetea maslahi mapana ya nchi yetu!! Kwa nini wabunge tusiwaite MANGUNGOS wa kizazi kipya?
 
T
Kiukweli zanzibar ipo, is why ina serikali yake, jeshi lao, mamlaka zao. Na wanajiita wanzazibar na wako proud kabisa
Wkt mtu wa mainland ukiija hivyo inaonekana kosa?
Huu muingano kama unapendelea one side
That's why nasema kwanza Tanganyika iwepo then wadai hiyo mali yake

Kuhusu muungano cha ajabu ni mainland ndio wanaun'gan'ganiaa wakati wala hauna faida nasi kuliko hao iasland, why? Why? Why?
 
sawa
sawa ila kuna kutangulia. amani ya nchi na usalama ni bora kuliko uhai wa mtu mmoja mjinga anaetaka sifa. hoja zake ashaambia selikali itazifanyia kazi.
Amani ipi? watanzania wanayo? ukweli, haki, na usawa ndio nguzo ya amani hii inamaana kuwa Uongozi wa Taifa ni uongozi wenye maoni ya ndio ya wengi sio kikundi Bora tukatolewa sadaka vizazi be yetu vikafurahia maisha sio kuongoza watu kama ng'mbe hatutakubali abadani.
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Mbona Kama unatishia kwani wewe siku zako hazihesabiki ama Ni milele utaishi. Kama kifo Ni ishu ya kawaida kwa kila kiumbe chenye uhai ama Kuna kitisho kingine zaidi ya kifo.
Sema Kama umekula hela za dp wedi
 
Hata akipata maneno yake ni sauti ya Tanganyika yataishi milele na ndio uharisia
 
Hii imekaa vizuri sana hii.
 
Huyu mjinga anatafuta sifa za kijinga. Play stupid games, win stupid prizes.
 
Hopeless thinking. Hujui chochote, unaropoka tu. Kwa fikra zako duni unaamini kwa kuwa katiba inasema Rais atakuwa amiri jeshi mkuu, basi ataamrisha majeshi yapambane na wanaotetea rasilimali za nchi?

Rais kuwa amiri jeshi mkuu ni katika kutoa amri kwa majeshi kunapokuwa na uvamizi wa mipaka yetu, na ku9nekana kuna haja ya kuingia vitani.napo ni baada ya ridhio la bunge.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Pole sana, umekuwa kama kasuku kila mahali unapeleka hoja zako hizi, ambazo zinajibiwa kikamilifu.

Kama wewe ndio wa kuonewa huruma sana, kwani mnalichukulia hili swala kama vile ni imani fulani ya kidini.

Hoja zako zote zimeshajibiwa zaidi ya mara elfu moja, unachokifanya wewe ni kuendeleza vurugu za kitoto..
 
kwa mfano, Kuna wizara ambazo sio za Muungano, na sio za Zanzibar. kwa maana hiyo, sio za Tanganyika??? anayekwambia Tanganyika haipo anakupotosha.


ndio maana mnakuwa na PM muongo muongo

YESU NI MASIHI
Ni za tanzania bara sio Tanganyika,
Tanganyika haipo, kwanini hamtaki kukubali ukweli? Nyerere aliiua tanganyika ili kuipata zanzibar, kwamba ana maslahi gani na zanzibar hilo sijui, ila hata wazanzibari hawautaki huu muungano, sasa swali ni kwanini wabara ndio wanlazimisha huu muungano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…