Taratibu mkuu 'cassavaleaves'.
Uamini wangu ni kuwa sasa tumefika pazuri kabisa pa kuung'oa mzizi.
Hapana. Nyerere hakutengeneza tatizo. Waliotengeneza tatizo ni hawa waliofuatia baada ya yeye. Muungano ulivyoanzishwa haukuwa na lengo la kufikia huku tulipo sasa. Hawa viongozi waliofuata chini ya CCM waliyageuza kabisa yaliyokuwa yamelengwa toka mwanzo kuwa matokeo ya muungano wetu.
Ili CCM iendelee kutawala kule Zanzibar, kila jambo lililodaiwa na kile kikundi kidogo cha waZanzibari, waliokuwa wakitishia kujiondoa kwenye muungano kila mara na kuibua kila aina ya zilizoitwa kero za muungano, walipewa zawadi ya rushwa, na CCM hii ili kuwanyamazisha. Haya ndiyo yaliyotufikisha hapa. Nyerere asingekubali upuuzi wa namna hiyo.
Sasa, nilisema hapo mwanzo, kwamba "sasa tumefikia pazuri" na muungano wetu huu, na ashukuriwe Mh. Samia Hassan Suluhu kutufikisha hapa tulipofikia, pengine bila yeye kunuia kufanya hivyo.
Sioni tena ni kwa namna gani, na nani anayeweza kuzuia uwepo wa Tanganyika tena. Hili halizuiliki tena, ingawaje halikuwa lengo, wakati muungano ulipo asisiwa.
Kalamu:
Nakushukuru mkuu kwa maoni yako, kwa upande wangu nilijua hakika DP World lazima serikali itaipitisha licha ya makandokando mengi yal0fichika humo! Na hata Maelezo ya Waziri muhusika, kwa upande wangu yameshindwa kuniridhisha, anyway mazungumzo yetu hapa ni Muungano, hayo ya DP tunaweza badilishana mawazo baadaye.
Ukweli wa mambo ni kuwa saga la DP World limefichua mambo mengi yaliyofichika ndani ya watu wa bara kuhusu Muungano, inawezekana kabisa kwa sababu za Kihistoria za wakati ule Nyerere na Karume walituungeneza huu Muungano. Lakini sababu hizo za Kihistoria hazipo tena! Sina haja ya kuzianisha hapa! Na hiyo miaka 60 hakuna KABISA JITIHADA ZA MAKUSUDI KUUREBISHA MUUNGANO UENDANI NA HALI HALISI YA LEO!
Kila ukiangalia hali yalisi leo, Hahitaji tafakuri kubwa, Muungano unapendelea kundi dogo mno la watu! Na watu hao wachache wa visiwani, wana nguvu kubwa MNO katika siasa ya Wananchi wa Tanzania Bara! Nguvu hiyo haipo kwa kiongozi wa bara katika Siasa za Zanzibari.
Mfumo huu wa sasa chini ya CCM, na kama ulivyo sasa hivi unaweza kumfanya Raisi akawa Mzanzibari, na akachagua kabisa Mawaziri wa wizara nyeti na taasisi muhimu kutoka Zanzibari kwa utashi wake, bila kuzuiwa na Katiba! Inaumiza mno! Raisi wa Muungano hawezi kuingilia taasisi za Zanzibari hivyo.
Na cha ajabu pia, ni kuwa hata huko Zanzibari, kama utafanya Referendum leo, na usipo ikwekea mizengwe Muungano unavunjika!
Mkuu Kalamu, nimefanya kazi na Wazanzibari wengi, nimezunguka karibu kila kona ya visiwa hivyo viwili, nimekaa vijijini! Ukweli ni kwamba hatupokelewi kwa mikono miwili watu toka bara! Tofauti kabisa na wao ambao wana uhuru wa kila aina huu upande wa pili!
Umsema kuwa mjadala wa DP World "sasa umetufikisha pazuri" kuhusu swala la kuungalia Muungano! Sidhani kabisa mkuu! CCM haiko hivyo, huwa haingalii mbele! Huwa haiwezi kujadili mambo magumu! Na kwa sasa hivi kuujadili Muungano, utakua uko kinyume na Mama! Hiyo ndio CCM! Inawezekana kuna baadhi ndani ya CCM wameona hilo, lakini nani ana uthubutu wa kusema lifanyiwe kazi! Jambia aliloshikishwa Raisi wa Tanzania ni kali sana! Ndani ya Chama na nje! Uhai kuwa mwanasiasa Tanzania unategemea hisani ya Raisi......Hivyo usitegemee mjadala wowote! Hili ni kongwa au mnyororo mzito wa kitumwa ambao watu wa bara tulivalishwa na Nyerere! Iko siku tutauvunja! Lakini sio leo.