Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi

Aisee

Wanasemaga mbuyu ulianza kama mchicha!

Mungu atutangulie ktk hili tutavuka salama

Mungu iongoze Tanzania, Mungu Ilinde Tanzania. #TanzaGiza!
Asanteni watangulizi wa JamiiForums.
The leaders of 2morro
 
KAULI YAKE NI JINAI TOSHA KABISA,HIZI NI KAULI ZA KUWAGAWA WATANZANIA NA KUHATARISHA MUUNGANO WETU NI ZA KUKEMEWA NA KULAANIWA IKIBIDI NA ADHABU YA KIFUNGO JUU,INFLICT,UCHOCHEZI,.
 
Umeamua kutoona mema ya CCM na ni mengi hivyo sina uwezo wa kubadilisha maoni yako mkuu cassavaleaves
Steven,

Kila ni kikaa na kutafakari mema ya CCM nashindwa kuyaona! CCM imetengeneza jamii ya Watanzania kuwa ya Kinafiki, uoga, kujipendekeza kwa wakubwa! Kuabudu viongozi, na kila mtu kujali tumbo lake!

Hali ya unafiki ni kubwa mno kwa Watanzania! Angalia maofisini, mnafanya kikao cha kawaida cha wafanyakazi, unauliza nani ana swali au nyongeza yoyote ile, unaona watu wako kimya! Ngoja watoke mlangoni! Manung'uniko, malalamishi chini chini, unabakia kujiuliza mbona hamkutoa madukuduki yenu kikaoni! Watanzania ni waoga mno kutoa mawazo yao! Tuliofanya kazi na Wakenya, Wanageria au watu wa West Africa na South Africa wako huru kutoa mawazo yao! Sio Mtanzania! Culture hiyo imejengwa na CCM! Kumuogopa Mkuu!

CCM imetengeneza Culture ya ulaji wa mali ya umma na ufujaji! Ni kama jadi kwa Watanzania! Mtu akipata kazi kubwa unasikia, kapata ulaji, na waharibifu wakubwa wa mali ya umma Tanzania, ukiondoa CCM yenyewe ni serikali ya CCM, tuliofanya na watendaji wa serikali , wakubwa kwa wadogo ni walafi wakubwa! Posho! Posho! (Per Diem) Mkutano mdogo wa kiofisi lazima kuwe na posho! Kitu hakiendi bila bahasha! Hili ni janga kubwa mno ambalo CCM imetujengea!

Janga jingine kubwa ni rushwa! .......Steven nisaidie kuyaoona hayo mema ya CCM unayoyazungumza!
 

Steven!

"Wakati wewe unaongelea benevolent dictactor wapo wanaoziona fursa nyingi za kibiashara na wanazitumia kikamilifu."

Ukijikomba kwa "Benevolent dictator" na mfumo wake utakosa fursa kweli! Umepofua macho yako! Kila kukicha Rostam Aziz na watu kama hao wanaingia Ikulu, unadhani wanakwenda kunywa kahawa? Ni kweli kina Rostam Aziz na kundi lao wanazitumia kikamilifu!
 
Wewe ni msaliti wa Tanganyika. Upi ukakasi wa maneno ya Mwabukusi?
 
"ashukuliwe" ndiyo nini kwenye heading hapo? Au mnaandika kwa lafdhi ya Kiarabu?
 
Hatari sana…….Wazanzibari wamelikoroga lazima walinywe
Hivi kama uwekezaji wa Bandari una faida kwa mkataba huu kwnn wasiwape DP WORLD bandari za Zanzibar?
 
Duuh....
Safi kwa kuanza kuelewa kinachopigiwa kelele.
Serikali imeshindwa vipi kuajiri hao wataalamu wa mataifa mengine yenyewe?
Huoni kuwa serikali imeshindwa kutuongoza nayo pia inapaswa ibinafishwe?
Serikali legelege ,haina uhalali wa kuwepo kuwepo kama inashindwa kusimamia kikamilifu eneo dogo tu la bandari , hiyo kampuni yenye watu wa kimafia wataiweza wapi .au ni yale mambo kila kitu SAA100 atakiona ikulu kama alivyosema
 
Naunga mkono hoja..
Inaboa sana kuongozwa na mtu ambaye hamkumchagua.
Kingine haya uliyopendekeza itakuwa ni njia nzuri sana ya kumlinda Rais aliyechaguliwa na watu ili hata makamu wake akiingiwa na tamaa ya madaraka, akate tamaa ya kufanya chochote kumdhuru kwa sababu kwa kufanya hivyo, hataweza kuchukua nafasi ya Rais, isipokuwa kwa ajili ya kulivusha tu Taifa kwa kipindi hicho cha mpito.
Ahsante sana kwa maoni mazuri Mkuu.
 
"Maliasili zetu Watanzania zinachukuliwa bure haya ni maajabu,sitaruhusu hilo" Hayati Rais John Pombe Magufuli.
 

Attachments

  • VID-20230715-WA0734.mp4
    9.5 MB
Unayo haki ya mawazo huru mkuu cassava. JPM hakuwa fascist. Alikuta taifa la wapigaji na akaamua alichangamshe.

Hakuna fascist anayeweza kujenga SGR kama ilivyojengwa na kuelekea kumalizika.

Hakuna dikteta anayeweza kupambana mpaka bwawa la Mwalimu Nyerere limekamilika na kwenda kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa.

Hakuna dikteta mwenye uwezo wa kufufua shirika la ndege na linapaa katika ushindani wa kidunia kwa kasi, hayupo mbabe wa aina hiyo.

Tunadhani ni dikteta kwa sababu wengi wetu tulizoea kubembelezana katika kila hatua ya uongozi wa nchi, tumezoea mno kupiga domo na kudhani wenzetu na wao wanaendekeza ujinga huu wa demokrasia zinazopitiliza kama sisi.

Muungano wetu sio fumbo la imani, mkuu usiikejeli imani katoliki hata kama wewe sio mkatoliki.

Muungono wetu umejikita kwenye utu wa mtu na hauwezi kukwepa mantiki ya muungano wakati wowote ule wa maisha yako. Usiwasikilize hawa wapumbavu wanaozungumzia Utanganyika katika afrika mashariki ambayo Sudan ya kusini inataka kuwa sehemu yake pia.

Usiwasikilize hawa wapumbavu wanaojiita watanganyika wakati Congo anaingia kwa kasi kuwa sehemu ya jumuiya ya afrika mashariki na kati.
 
Tatizo letu kubwa ni elimu tu. Mengi yanayoendelea katika mijadala ya mitandaoni ni ushahidi wa upungufu wa elimu tulionao.

Mengi yanayohusu bandari ni ukosefu tu wa elimu ya kisasa. Ushahidi ni namna wanasheria walivyoweza kujibu hoja zote zilizoletwa kuhusu bandari siku walipofanya mkutano na waandishi wa habari.

Tusichezee elimu, kwa kufanya hivyo tunazalisha wajinga wengi sana, wanaoweza kudanganywa kwa hoja nyepesi za mtu mwenye nia mbaya.

Culture ya ulaji hata hao CHADEMA wanayo. Hata huo upinzani kwa ujumla umejaa hiyo culture.

Mengi unayoandika ni malalamiko tu, ni hisia zako japo unaruhusiwa kuwa nazo.
 
Mkuu unalialia sana. Huyo dikteta ndio kiongozi wako na huna mwingine sasa unafanyaje ili uweze kuishi?.

Nenda kapige kura siku ya uchaguzi uweze kuchagua unayemtaka. Kulalamika hapa JF bila ya kutafuta suluhisho katika sanduku la kura ni kupoteza muda tu.

Unaishia kuwa mwanaharakati fulani mwenye hasira muda wote.
 

Usiniingize Chadema kwa nguvu!...Sina kadi yoyote ya Chama chochote Tanzania.....Ni Mtanzania naipenda Tanzania.....Hayo mawazo zuzu kila anayetoa hoja dhidi ya CCM ni Chadema ndio ujinga wa wana CCM!
 
Naona unashindwa kunielewa na hutanilewa! Sijahishi Tanzania hata siku moja kwa Hisani ya CCM! Akili za Watanzania wengi CCM ndio Baba, CCM ndio Mama....CCM ndio "mungu"
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.

Hata wewe hauwezi kuepuka kifo.

Jaribu kuficha upumbavu wako kwenye mambo muhimu ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…