Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Maneno mazito mno,
Nina uhakika huko ndani sasa hv wanatafutana kwa fukuto, punde kuna watu hawataweza kabiliana na hili fukuto na hapo watajitenga, wazalendo watagoma kuchangamana na wezi na mpasuko utaanzia hapo!
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Halafu inaonekana hata sheria hajui, Tanganyika haipooooo
Halafu hili jina hili tz hakuna majina ya hivi
 
Daah Jamaa anaongea hadi unaogopa VOCAL ya hatari ina bonge la Punch ,lazima waelewe tu.

Watu wanashindwa kutofautisha nini waTZ wanataka ,tatizo siyo DPW world kuwekeza Bandarini tatizo ni Kwenye mkataba wa kichifu mangungo wa kuuza bandari tena wauzaji wa mali za tanganyika ni kina AMIJEI.
Watoto lainilaini wapenda mshedede wapenda masihara ya kifedhuli wanatuuza kweli miguvu sio kila kitu.
 
huyo mbwa kuna kitu kinamwasha siku si nyingi atapata anachokitafuta. Ameshindwa kupata umaarufu huko mahakamani kwasababu ni kilaza. Amekula pesa za mafisadi wanaofikiri wanaweza kuikwamisha serikali hii, atakwama yeye ngedere. Lengo la hao mambwa ni kuikwamisha serikali na wanatumika na mafisadi wa bandari. Mnafiki mkubwa eti Tanganyika yetu, anaijua Tanganyika huyo fala? Hii nchi haigawanyiki watagawanyika wao.
At least he's trying to address the elephant in the room, what have you done?

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Ulimboka mtupu zaidi anaongea kwa jazba huyu jamaa.

"Uongeeni ukweli hata kama ni mchungu kiasi gani kwa watawala"

Wanahitajika akina Mwambukusi zaidi ili kunogesha mjadala wa Tanganyika yetu.
 
huyo mbwa kuna kitu kinamwasha siku si nyingi atapata anachokitafuta. Ameshindwa kupata umaarufu huko mahakamani kwasababu ni kilaza. Amekula pesa za mafisadi wanaofikiri wanaweza kuikwamisha serikali hii, atakwama yeye ngedere. Lengo la hao mambwa ni kuikwamisha serikali na wanatumika na mafisadi wa bandari. Mnafiki mkubwa eti Tanganyika yetu, anaijua Tanganyika huyo fala? Hii nchi haigawanyiki watagawanyika wao.
Mwanasheria gani hata hajui kama Tanganyika haipo?
 
Daah nilikua nafikiria mchana badala ya viongozi kutengeneza Ajira za vijana kupitia hata hiyo Bandari wao wapo busy kuuza unawakuta mtaani wengine wapo na boda boda na degree zao huku watoto wa Bandari wakipepa tuu...
 
Hii article imejisimamia!
Inasomeka na inaeleweka kuanzia makao makuu ya akili na Uzalendo.

Kwamba kila nchi ijisimamie.

Hii ina Maanisha Zanzibar inaye Rais, Tanganyika haijafanya Uchaguzi.

Kipindi kigumu sana hiki.

Katiba Mbovu.

Rais akifia Madarakani yapaswa baada ya kipindi kifupi kama 90 days ufanyike uchaguzi, na anayekaimu nafasi ya rais aliyeaga dunia ndani ya siku 90 asiruhusiwe kufanya mabadiliko ya nyadhifa zozote ndani ya utawala uliokuwepo. Na hakuna kusaini mikataba ya uwekezaji mpaka uchaguzi.
Katiba yetu ndiyo inasema hayo uliyoyaandika hapo chini au umetoa maoni yako kuhusu katiba inavyotakiwa kuwa?
 
Back
Top Bottom