Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Ali Karume kasema Hussein Mwinyi mtanganyika anauza mali ya Zanzibar. Kwa habari za mitandao wanasema yupo chini ya ulinzi Msasani
Ali Karume nae ni Mnyasa wa Malawi, Zanzibar haina mwenyewe japo wakazi wa huko wanajishau kuwa ni yao, Wazanzibar wote ni wahamiaji, wametoka bara na nchi za jirani wengine wametoka kwa wajomba zetu Uarabuni,wengine Comoro ,China ,India. Zanzibar wapoWasukuma ,Wanyamwezi,Wadigo,Wakwere,Wanyakyusa, Zanzibar haina mwenyewe hata hawa akina Jussa ni wahindi weusi.
 
Ila kuongea ukweli unawaacha serikali uchi ,wanadhani wametukanwa
Wakili Boniphace Mwabukusi amekuja kwa ghafla. Huyu ndiye man of the moment. Anaongea kwa mode ya kiuchungaji kwa kufoka anapojenga hoja zake.

Anyway ngoja tuone hatma yake japo kazidisha matusi na dharau
 
Nimemwona jana Masauni kwenye taarifa ya habari akipiga mkwara kwamba watu wasitumie uhuru wa maoni vibaya, nikajiuliza kumbe kutumia uhuru wa maoni vibaya ni kupinga kuuzwa kwa bandari zetu ambazo kimsingi ni mali za wananchi wa Tanganyika?

Bandari za Tanganyika ni mali ya wananchi wa Tanganyika na ni roho ya uchumi wa Tanganyika, inakuwaje ghafla mwarabu ndo apewe haki ya kumiliki bandari za Tanganyika huku mtanganyika abaki na wajibu wa kumrahishisa mwarabu kuendelea na uwekezaji wake wa milele?

Wananchi wanapotoa maoni ya kupinga rasilimali zao kuuzwa au kugawiwa kwa wageni bila ridhaa yao kwa nini hilo litafsiriwe kama kutumia vibaya uhuru wa maoni? Hii haiwezi kuwa haki hata kidogo.
 
Kulipwa malipo mpeleke takukuru,ukiwa umejipanga na fact za kisayansi na sio maneno kutoka kwenye hewa

Alikuwepo ila kapokea malipo unadhani hizi kelele anapiga sababu mzalendo sana? pesa bwana hakuna asiyejuwa anafanya kazi aliyolipwa kama mzalendo ndio leo? siku za watu wenye roho wasiokuwa na uhuruma walikuwa wapi? Mama Samia huu upole utamponza nchi haiendi hivyo JPM alijuwa kuwanyosha hawa.
 
A
Acheni kukumbatia makaa ya moto, ni muda sasa wa kuruhusu watu wajadili huu muungano na katiba kwa ujumla tunakoelekea tutakuja kushtuka mambo yakiwa ni magumu zaidi, serikali tatu ni suluhusho. Mengineyo huko mbele ya safari mtawaua wengi
Mambo mengi hayatakiwi kujadiliwa kwa ujumla wake hadharani kwa sababu za kiusalama.
Hata hivyo, tunahitaji viongozi smart kwa Muungano imara na Mustakabali mwema wa Tanzania.
Siasa zetu zimejaa ujinga na hivyo hoja hujibiwa kijingajinga.
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Chama cha Mapinduzi kinahitaji kutumia watu wenye akili nzuri, busara na weledi kujibu hoja za msingi. Comedians watumike kwa burdani tu.
 
Hata Dunia izunguke mpka ifyatuke Raisi kama Magu hawez tokea Tena
, Wakili anaongea fact tupu ucdhan hakuna anae elewa wote wanaelewa vyema lakn shida hofu waaliojengewa wananchi wanaona kama vile hawan haki ya kuuliza kuhusu rasilimali zao, every Tanganyikan is fully responsible to inquire anything concerning Tanganyika
NI upuuzi kuja kuruhusu atokee tena rais wa aina hiyo
 
Mtu Msomi halafu kijana hapaswi kuongelea Mambo ya Utanganyika tena zama hizo!

TANZANIA NI MOJA NA MUUNGANO NI KITU CHEMA!

Hoja zake zingeweza kuwa na nguvu lakini kitendo cha Kuegemea kwenye Utanganyika na Uzanzibari kuharibu kila kitu!

Hana Hoja!!!
Kama Tanzania ni moja kwanini Zanzibar wanajitambulisha kama nchi?
Muungano gani Mtanganyika anabaguliwa Zanzibar hasa kwenye ajira na umiliki wa ardhi?

Katika muungano huo kulikusanywa maoni ya wananchi kuwa wanauhitaji?

Itoshe kusema kwamba huu muungano ni wa viongozi na sio wa wananchi.
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Mwehu huyu. Anajilengesha ili akijikwaa tu akaanguka aanze kuleta ngonjera za akina Nshalla kuwa anataka kuuawa.
 
Aisee

Wanasemaga mbuyu ulianza kama mchicha!
Nikuulize wewe unaweza kujua hili:
Kamati Kuu ya CCM ina wajumbe wangapi toka Zanzibar?

Inavyo onekana sasa hivi ni kuwa CCM Zanzibar ndiyo inayoendesha maswala yote yanayoihusu Tanganyika.
Inabidi sasa hili nalo tulitambue vizuri.

Nitumie fursa hii pia, kusema kwa uhakika kabisa, kwamba Samia ndiye atakayekuwa mZanzibar wa mwisho kuitawala Tanganyika. Haitatokea tena mwingine.

Mkuu 'johnthebaptist', nasubiri jibu la swali langu.
 
Back
Top Bottom