Wakili Boniface Mwabukusi: Hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya ovyo kwenye Mali za Tanganyika

Tangu tupate Uhuru wangetokea wawili tu wenye ujasiri kama huyu Naamini mpaka sasa China ikasoma kwa maendeleo ambayo tungewazidi.

Tatizo kubwa la hii nchi ukute hapo anaongea sana na Watanzania wengi kumsikiliza na kumuamini kumbe kuna miamba ya kona Kona yenye mirija pale bandarini wamemtanguliza tu mstari wa mbele kimgambo
Umeelewa hata anachopinga?

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Wakili Boniface apewe ulinzi ,asiwaamini tena watu wake wa karibu wasije kumpa Polonium210.

Huyu Jamaa alikuwepo wapi siku zote? Alichelewa sana Kuja ,ndiyo maana tunasema hauwezi kuzuia watu kusema kwa kuua ,ukiua mmoja anazaliwa mwingine ,wamemuondoa Ben Saanane lakini wapo watu wanakuja mwendo wa ngiri mkia juu.
Dah!

Hilo la "ngiri na mkia juu" umechora picha isiyosahaulika kirahisi.

Huenda unakipaji cha kufundisha vizuri sana, bali hukitumii hicho kipaji ipasavyo.
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Mpumbavu sana huyu Mwabukusi. Nyakati za JPM asingethubutu kufungua mdomo wake kama anavyofanya muda huu.

Siku nyingi tu tungekuwa tumesaini mikataba ya uwekezaji pale ikulu na media zote zingeimba mapambio. Leo anaongea kwa sauti ya juu ni kwa sababu mamlaka za juu zimempa uhuru wa kufanya hivyo.
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Amiri jeshi mkuu Mtanganyika?
 
Amechelewa sana na hataweza kumzuia Mzanzibar mwingine yoyote yule endapo kama atajitokeza mwingine ambaye anataka kufanya hayo yaliyofanyika.
Suluhisho pekee la kudumu ni wananxhi wenyewe wa Tanzania kushikamana kwa pamoja na kupigania upatikanaji wa Katiba Mpya itakayotokana na mawazo au maoni yao wenyewe wananchi.
Nikueleze kwa uhakika kabisa, Samia ndiye mZanzibar wa mwisho kuitawala Tanganyika. Hatatokea mwingine tena.

Hili unaweza kulipeleka benki ukadai kitita juu yake jinsi lilivyo la uhakika kamili.
 
Hii article imejisimamia!
Inasomeka na inaeleweka kuanzia makao makuu ya akili na Uzalendo.

Kwamba kila nchi ijisimamie.

Hii ina Maanisha Zanzibar inaye Rais, Tanganyika haijafanya Uchaguzi.

Kipindi kigumu sana hiki.

Katiba Mbovu.

Rais akifia Madarakani yapaswa baada ya kipindi kifupi kama 90 days ufanyike uchaguzi, na anayekaimu nafasi ya rais aliyeaga dunia ndani ya siku 90 asiruhusiwe kufanya mabadiliko ya nyadhifa zozote ndani ya utawala uliokuwepo. Na hakuna kusaini mikataba ya uwekezaji mpaka uchaguzi.
I love this good thinking 🙏🙏🙏
 
WAKILI BONIFACE MWABUKUSI;KAMA HAMTATUSIKILIZA,TUTAZUNGUMZA LUGHA MTAKAYOTUSIKILIZA,HATUTARUHUSU MZANZIBARI KUFANYA MAMBO YA HOVYO KWENYE MALI ZA TANGANYIKA.

"Wazee wangu wa Mbeya nipo hapa kuwahakikishia Tanganyika hailiwi tena,tutafuatilia hatua kwa hatua kwenye mikataba ya Mali zote za Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba unatakiwa ujisimamie na ujitetee,ila watu wanautetea bila "baseline" za data na facts kwenye mkataba huo,hakuna research wala data, mkataba hauna data ambazo ni measured kisayansi watu wanacheza na maneno tu ambayo hayapo kwenye mkataba" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mkataba wa bandari ni batili, chochote kilichofanywa nje ya sheria na nje ya katiba kirekebishwe" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar,hatutaruhusu Mzanzibari kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Tanganyika,kama ambavyo Mtanganyika hawezi kufanya mambo ya hovyo kwenye Mali za Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ndoa ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ndoa ya utotoni sasa tumekua tunataka tuongee tukubaliane Mali za Tanganyika ziwe chini ya Mtanganyika na Mali za Zanzibar ziwe chini ya Mzanzibari" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu alitudanganya kuhusu kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli na hajawahi kuomba radhi,na leo anatudanganya kuhusu mkataba wa bandari,akae pembeni kumsaidia Rais" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu atujibu,sheria sura 449 na sheria sura 450 kuhusu Ulinzi wa rasilimali za nchi na kuhusu ushughulikiwaji wa vifungu vyenye utata walizifuata,je vipengele vya mkataba wa bandari vinaoana na vipengele hivi vya sheria yetu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Waziri Mkuu atujibu,kwa nini bunge linataka kubadili sheria sasa hivi ziendane na mkataba huu wa bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tuliibinafsisha Tanesco kwa Net Solution tulipata faida gani na leo Tanesco ya nani? Tulileta watu TRL wakaishia kubeba vichwa vya treni kurudi navyo India,tulifanya hivyo hivyo kwa NBC kuuzwa bei ya kutupwa,na leo mnatuambia mna muujiza kwenye kuibinafsisha bandari" Wakili Boniface Mwabukusi

"Kama mkataba ni sahihi,Waziri Mkuu anatuambiaje tukusanye maoni,nani anakusanya maoni,yaende wapi,ya nini? kama mkataba tayari umeshapita" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wakati nchi yetu ina Kiongozi mwenye element za Uzalendo watu fulani hawakuonekana kabisa,sasa hivi wamerudi wanatukana hadi Mahakama, Watanzania angalieni walioko nyuma ya huu mkataba"Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kila uovu juu ya Tanganyika tutaukabili kwa jina lake na kila muovu tutamkabili kwa jinsi anavyokuja,hii ni nchi yetu hatutamuchia mtu mwingine aitetee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mabadiliko ya sheria yanayokwenda kufanyika ni matusi kwa Tanganyika,narudia tena Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Tunatoa onyo kwa Kiongozi mwingine kudhani anaweza kuingia mikataba ya kuuza nchi akabaki salama,wasituchezee" Wakili Boniface Mwabukusi

"Tunawaomba Watanzania wa dini zote,Waislamu, Wakristo,Wachungaji na Mashehe na WA jadi,tufunge tarehe 14,15,16 kuomba mapenzi ya Mungu yakafanyike kwa Tanganyika na Tanzania,ahsanteni sana"Wakili Boniface Mwabukusi
Safi kabisa wakili Mwambukusi.
 
anachokitafta atakipata. soon atajua maana ya amri jeshi mkuu inamaana gani. ngoja aendelee kufurahisha genge. his days are numbered.
Mentality ya kijinga sana hii,usitishe watu,toa hoja yako ipambane na hoja zake!
 
Wakili Mwabukusi hapo amezidisha ukali wa maneno na matamshi yake, tena sana. Mpaka roho imenistuka dah!!!

Hata viongozi wa vyama vya upinzani kina Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Zitto Zuberi Kabwe, Yuda Iskarioti (Prof Lipumba) hawajawahi kutoa matamshi makali kiasi hicho!

Sisi wengine kila kukicha tunaitoa kasoro Serikali, Mawaziri na CCM kwa maamuzi wanayofanya, tokea enzi za mwendazake. Kila siku tunavurugana nao mitandaoni... Ila hatujawahi kuthubutu kufikia kutoa maneno makali na yenye ukakasi kiasi hicho!

Mungu iongoze Tanzania, Mungu Ilinde Tanzania. #TanzaGiza!

Mkuu,

Ukakasi uko wapi hasa.....? Nimeisikiliza hotuba nzima, Watanzania hawapendi viongozi kuambiwa ukweli...Kasema Waziri Mkuu asiaminike....Wewe una mwanini Waziri Mkuu? Kadanganya katika mambo mengi....! Kama ungeweza kupata hotuba wakati wa kupigania uhuru wetu....Ukiwasikia akina Bibi Titi na wengine wengi, labda ungekuja na mawazo tofauti! Nisaidie Mkuu kuhusu ukakasi wa Mwabukusi......labda sikumuelewa...
 
Hakuna jipya hapo Nyerere alishayaona haya..mkipata Tanganyika mtaanza huyu dini gani..huyu wa kanda gani?..dhambi ya ubaguzi haijawahi kumuacha mtu salama

Unataka Watanganyika wabaguliwe mara ngapi! Mkataba wa DP wenyewe umeitenga Zanzibar isihusike....ila kama ina faida itaingia kwenye kapu la Muungano...Huoni ni ujinga mkubwa Mkuu...! Nena Zanzibar utajua maana ya Ubaguzi...
 
Hahahahah kumbe watu bado mna akili za hovyo kiasi hiki. Sasa alichokosea ni kipi huyo bwana. Ametoa maoni yake kama raia wa Kitanzania. Ama uhuru wa maoni hakuna tena kwenye awamu hii kama mlivyojinasibisha awali?

Mkuu,

Watanzania tuna safari ndefu ya kuleta mabadiliko Mkuu.....Serikali na viongozi ni miungu.....hawakosei...na hawataliwi kuguswa!
 
Back
Top Bottom