Hata akija rais mwanademokrasia bado kulalamika hakuishi!, lakini cha muhimu ni uhai.
Unaona yaliyompata Sozigwa? Hiyo ndio CCM...
Paulo Sozigwa, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Rais Julius Kambarage Nyerere, anakabiliwa na hali ngumu kimaisha.
Sozigwa, ambaye kwa sasa anaumwa ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), anaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu, akisaidiwa na familia yake na wasamaria wema.
Kutaabika huko kumechangiwa na kutopata malipo ya kiinua mgongo na pensheni, kwa kile kinachoelezwa kwamba ni kutokuwapo kumbukumbu zake za kiutumishi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ofisi Binafsi ya Rais hadi serikalini ambako aliwahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utalii.
Katika mahojiano maalumu yaliyofanywa na JAMHURI nyumbani kwake Magomeni Mapipa, Dar es Salaam, mke wa Sozigwa, Monica Kuga, anasema hali yao uchumi ni mbaya kiasi cha kumfanya amtunze mumewe kwa misaada kutoka kwa jamaa na watu waliomfahamu vizuri enzi za utendaji kazi wake.
Wakati Mama Kuga akisema kinachowataabisha ni kukosekana kwa mafao na pensheni, baadhi ya watu waliozungumza na JAMHURI wanasema, kilichomponza mwanasiasa na mtangazaji huyo mahiri wa redio, ni kazi yake aliyoifanya akiwa katika Kamati ya Maadili ya CCM.