Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
"Rushwa ukiitazama katika mfumo wa kijinai tunasema unapaswa uthibitishe pasipo na shaka lakini mkija kwenye upande wa chama kama CHADEMA, kwanza tunapaswa kujuwa kuwa CHADEMA ni tumaini la Watanzania kwa hiyo wanapaswa kujuwa kuwa hawapaswi kutiliwa shaka hata kidogo, ni kama tunavyosema mke wa Kaisari yaani hupaswi kumtilia shaka kwa sababu ndio tumaini, na CHADEMA imejijenga katika kupambana na rushwa, watu wanawapenda kwa sababu walitoka nje wakasema na kuonekana wanapambana na rushwa, walikuwa wanapinga mafisadi watu wakasema hiki ndio chama, sasa kama sasa kuna viashiria vya rushwa au tuhuma za rushwa hili sio jambo jema kwakweli, na sio jambo jema pia kusema kuna rushwa ndani ya chama halafu inakaliwa kimya yaani haichukuliwi hatua sio sawa" -Wakili Jebra
"Mimi siwezi kuzungumzia ajenda za Kamati Kuu huko sijuwi kwa sababu sikuwepo, sijuwi kama (Tundu Lissu) aliomba msamaha au la siwezi kuzungumzia kwa sababu sikuwepo, sijaona muongozo au minutes za vikao na wenyewe wametuambia ni siri za Kamati Kuu, lakini jambo ninalotaka kusema ni kwamba chama cha upinzani ambalo ni tumaini la Watanzania wanapaswa kuwa wasafi zaidi ya vyama vingine, tena zaidi hata ya chama tawala, yaani kinapaswa kuwa pale juu kwa sababu watu wanajuwa kuwa hawa ndio watu ambao tunawategemea, lakini kama taarifa zinatoka kutoka kwa Makamu Mwenyekiti, viongozi na wanachama kuwa kuna watu wanaweza kumchukua mtoto wa Rais (Abdul) na kumpeleka kwa kiongozi kwa njia ya mikato hilo linatia mashaka sana" -Wakili Jebra
"Kiongozi wa chama cha upinzani hauwezi kutoka mbele na kujinasibu kuwa mimi nilimchukua mtoto wa Rais au mtoto wa fulani, nikampeleka kwa fulani ili amsaidie kufanya vitu hivi na hivi, wanatakiwa wawe kama mke wa Kaisari yaani wasafi hata mashaka huna, lakini kwa story zinazoendelea, conversation zinazofanyika hazina afya kwa chama cha upinzani kinachoaminika kuelezwa kuwa kashfa za rushwa, na rushwa zinazotajwa hapa inawezekana zina ushahidi au hazina lakini ukiunganisha mambo unaona hapa kuna mashaka"
Jambo