Jebra Kambole kawazidi kwa pamoja "CCM/SERIKALI/NEC/ZEC/BUNGE" akili na maarifa, aliliona hili muda mrefu ila alisubiri kufanya mapingamizi ya kuzuia uchaguzi mkuu ndani ya muda mfupi sana uliobakia kufanyika (Siku 7).
Ninacho kiona, mahakama ya africa iliamuru na itaamuru sheria ibadilishwe kama hukumu ilivyotaka kabla ya uchaguzi huu, kwasababu serikali haina sababu za kujitetea kwa kutotekeleza maagizo ya hukumu ile kwa miaka 9 (Tokea 2011). Lazima sheria ibadilishwe iruhusu mgombea huru, na ndio mchakato wa kutangaza nia na kuchukua form uanze tena upya.
HAPA KUNA MAWILI:
1) Serikali ya jiwe ikubali kuahirisha uchaguzi na kufanya kwanza mabadiliko ya Sheria ya kugombea ili iruhusu mgombea huru kama hukumu ilivyotaka.
2) Serikali ikaidi kwa "MABAVU" kutekeleza maagizo ya hukumu ile ya mahakama ya africa.
La kwanza likitekelezwa, basi CCM wana changamoto kubwa sana katika uchaguzi utakaofanyika baada ya kubadilishwa sheria ya uchaguzi (Sheria itawabana na kuwapunguzia nguvu na wengi watakimbia chama baada ya kukatwa mikia). Serikali pia itakutana na changamoto kubwa zaidi baada ya kutumia tayari mabilioni (Fedha za walipa kodi) kujiandaa vikali na uchaguzi huu na kisha uchaguzi kutofanyika, ukizingatia serikali sasa haina fedha (Serikali itaingia gharama mara mbili kufanyika kwa uchaguzi mmoja, kwa fedha za ndani).
Serikali ikikubali kupokea msaada kutoka mataifa ya nje au UN, basi uchaguzi utakua na usimamizi mkali sana kutoka kwa mataifa ya nje/UN.
La pili, serikali ikikaidi kwa mabavu kutekeleza maagizo ya hukumu, kwa kubadili sheria kwanza ndio uchaguzi ufanyike, kisha ikasema uchaguzi upo pale pale na sheria haibadilishwi. Basi "UMOJA WA AFRICA/UMOJA WA MATAIFA/UMOJA WA NCHI ZA ULAYA/MAREKANI/UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI" watatoka na tamko moja. Tamko litakua "HAWAMTAMBUI RAIS WA TANZANIA".
NB: Serikali itumie busara kwenye hili, akisikilizwa mmoja tu kwa kufuata matakwa yake anayotaka basi ataiponza nchi yetu pendwa.