mkongoman leo
JF-Expert Member
- Mar 26, 2026
- 294
- 345
Katuga kaingiza siasa kwenye kesi hii na porojo za mitandao irrerevant questions
hii kesi ni ya mchongo from the beginning, kwa hiyo lazima iwe hivyoSisi tulitegemea ungefanya kazi ya maana ya kwenda kuisaidia mahakama kutenda haki lakini tunachokiona, wewe unaenda kuleta udaku, kuzungumza vitu visivyohusiana na mashitaka. Kiufupi unapoteza muda wa majaji na unakuonyesha kuwa inabidi labda urudi shule kuongeza ujuzi wa sheria.
Sasa Passport ya Shahidi inahusiana nini na mashitaka yaliyo mbele ya mahakama?
Kwamba Shahidi anakwenda Dubai na kulala hoteli nzuri yanaisaidia vipi mahakama kutenda haki?
Kwamba shahidi ana magari mangapi yanawasaidiaje majaji kuthibitisha hati yenu ya mashitaka?
Tulitegemea ujenge ushawishi kwa majaji kuwa mtuhumiwa aliposema atahamasisha uasi basi alimaanisha uasi wa kihaini na si uasi wa kupinga mifumo kandamizi kama baba wa Taifs alivyowahi kuwausia vijana wafanye.
Tulitegemea uishawishi mahakama kuwa mtuhumiwa aliposema tutakinukisha alimaanisha kuinua silaha dhidi ya Jamhuri, au kushirikiana na adui wa nje dhidi ya Jamhuri, au kumdhuru rais wa Jamhuri au kuiondoa serikali kwa nguvu. Tulitegemea uishawishi mahakama kuwa neno kukinukisha ni Kisawe (Synonym) cha Uhaini na kwamba halina maana nyingine yoyote zaidi ya hayo au kwamba haliwezi kutumika kwa kitu kingine chochote zaidi ya hicho!. Tulitegemea uishawishi mahakama kuwa kukinukisha haiwezekani kwenye kitu kingine chochote isipokuwa kwenye uhaini. Sisi wapenda sanaa mara kibao huwa tunaongea mitaani kuwa Harmonize Kakinukisha ile mbaya kwenye show yake, Au Mithun alikinukisha vibays kwenye movie ya Disco Dancer, au Anold Shwazinegger alikinukisha kinoma kwenye movie ya Terminator. Hebu ishawishi mahakama ikuamini kuwa kukinukisha lazima tu uipindue serikali au uitishe serikali.
Tulitegemea uishawishi mahakama kuwa mtuhumiwa aliposema tutavuruga chaguzi hakuwa na maana nyingine yoyote isipokuwa kuitisha serikali, kwamba huwezi kuvuruga uchaguzi kwa kushawishi wananchi kisiasa kutumia haki yao ya kushiriki au kutoshiriki mambo ya siasa kwa kugomea uchaguzi huo na hivyo kuuondolea uhalali wa kisiasa.
Hayo ndo mambo sisi wananchi wa Jamhuri tunaokulipa mshahara kupitia kodi zetu tulitegemea kuyasikia ukiyajengea ushawishi hapo mahakamani na siyo udaku wa Heche ana magari mangapi, kalala hoteli gani, passport kapewa na nani. Hayo kwa maoni yangu ni matumizi mabaya ya muda wa mahakama na Jamhuri.
Hebu tusaidie haki itendeke hapo mahakamani achana na porojo!