Wakili Kibatala: Nitatoa taarifa rasmi kuhusu Askofu Gwajima Saa 11 Jioni

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
“Nimeona hiyo karatasi lakini inamtaja mteja wangu Askofu Josephat Gwajima nitatoa taarifa rasmi saa 11 ya kisheria na nini kinafuata lakini ni mwaka wa kuchoka sana, kuchoka mwili na kuchoka roho pia lakini Mungu wa mbinguni atatutia nguvu”

Ni maneno ya Wakili Peter Kibatala ambaye ni wakili wa Josephat Gwajima(Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima) akizungumza na Jambo TV leo Novemba 08, 2025 baada ya kupata taarifa kuwa mteja wake ni miongoni mwa wanaotafutwa ili kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini kwa madai ya kuhusika kwake kupanga na kutekeleza vurugu zilizotokea nchini Oktoba 29, 2025.
Your browser is not able to display this video.

Source Jambo TV
 
Mama kama kweli ana taka maridhiano atoe msamaha Kwa wote kuanzia viongozi wa upinzani mpaka wananchi waliokamatwa sababu ya maandamano.kama makosa WOTE TUNA MAKOSA serikali na wananchi pia.ni muda wa kuanza upya.
Lakini lazma wakae wafanye reforms ambazo wapinzani wanataka.tunajua ccm hawawezi kuachia ikulu lakini hivi ni kweli Kuna lazma mwenyekiti wa serikali za mtaa awe ccm,mbunge awe ccm diwani awe ccm?Tena Kwa kura za wizi?
 
Hakuna maridhiano na hao watu hawahitaji msamaha wa mzanzibar
 
Kumbe kuna muda una akili timamu mkuu.
 
Changamoto itakuwa akibanwa kwenye utekaji. Je atakuwa tayari kumtosa mwanaye Abdul kama kiongozi wa kundi la Watekaji kwa maana ni lazima Mafwele atamtaja tu?

Pia suala limekuwa gumu baada ya mauaji. Je atakuwa yupo tayari kuwa responsible kwa mauaji kama Amiri Jeshi Mkuu?

Ugumu upo hapo ila hayo mengine yanawezekana kabisa bosi japo inafikirisha.
 
Akiamua kufanya suluhu ya maridhiano anatakiwa akomeshe na hilo.maana nalo ndo chanzo Cha yote haya.mtu kama mzee kibao anashushwa kwenye gari anakwenda kuuliwa na kutupwa ununio alafu mpaka Leo hakuna uchunguzi wowote ni jambo linalompa sifa mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…