Wakili Kisabo: Jeshi la Polisi litoe taarifa rasmi kuhusu alipo kada wa Chadema, John Pambalu

Wakili Kisabo: Jeshi la Polisi litoe taarifa rasmi kuhusu alipo kada wa Chadema, John Pambalu

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Wakili Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu alipo John Pambalu, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye anadaiwa kukamatwa na maafisa wa Jeshi la Polisi jijini Arusha na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Soma pia CHADEMA: John Pambalu akamatwa na kupelekwa Central Police Arusha

IMG_3783.jpeg

Pichani: Wakili Paul Kisabo​

Kisabo, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utetezi wa THRDC, ametoa wito huo leo, Oktoba 15, 2026, baada ya kufika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station) jijini Dar es Salaam kufuatilia suala hilo. Hata hivyo, amesema hajapata majibu kuhusu mahali alipo Pambalu.

“Nimefuatilia suala la Mwalimu John Pambalu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police Station), Dar es Salaam, tangu saa tatu asubuhi leo, Oktoba 15, 2026, lakini sijapata majibu kuhusu mahali alipopelekwa Pambalu. Natoa wito kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu alipo ili apate uwakilishi kamili wa kisheria. Mchana huu natoka Central,” amesema Kisabo.

1792083643954.png


IMG_3784.jpeg

Pichani; John Pambalu anayedaiwa kukamatwa ​

Ikumbukwe kuwa Oktoba 14, 2026, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Yohana Kaunya, alieleza mbele ya umma kuhusu tukio la kukamatwa kwa viongozi kwao, akiwemo Mkurugenzi wa Mafunzo, Oganaizesheni na Uchaguzi, John Pambalu. Katika maelezo hayo, ilielezwa kuwa Pambalu alipelekwa Dar es Salaam.
 
Duuuh! Si walisema alipewa Wito na ZCO? Wamuulize vizuri huyo ZCO anajua aliko Pambalu.
 
Back
Top Bottom