Wakili Madeleka: Hauwezi kuwa na Vyama kwenye nchi isiyo na Haki

Wakili Madeleka: Hauwezi kuwa na Vyama kwenye nchi isiyo na Haki

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Wakili Peter Madeleka, amesisitiza kuwa udhibiti wa haki za kimsingi nchini haupaswi kuangaziwa kwa jicho la kisiasa au vyama, bali kama suala la kitaifa linalogusa kila mwananchi na Katiba ya nchi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha Mwananchi Digital, 8August 2026, Wakili Madeleka ameeleza kuwa siasa na shughuli za kisiasa haziwezi kunawiri katika mazingira ambayo misingi ya haki imemomonyoka.

"Haki sio chama, na ndio maana unaona watu wamejikita sana kuuliza 'sasa unaenda chama gani?'. Hapa hatuzungumzii swala la chama; hauwezi kuwa na chama katika mazingira au nchi ambayo haina haki," amesema Wakili Madeleka.


 
Katiba ataidai nani kama hakuna vyama. Au hujui cornerstone/ significance ya vyama. Mkiwa wengi mkapaza sauti madhulumati yataanguka, peke yako watakumaliza
Hao wengi unaowasema watakutana wapi kama hakuna haki ya kukusanyika?
 
Ndipo hapo nguvu ya umma inatumika, sharpaville massacre and the like mpaka mnatoboa. It is a hard way to go indeed
Sharpeville ilileta haki au ilileta umwagaji damu? Umesahau kuwa baada ya pale ANC ilipigwa marufuku na Mandela akafungwa?
 
Haki ni kwa wewe kuwa Rais au nini Bwana Madeleka.
 
Back
Top Bottom