Wakili Madeleka tusaidie kwenye kufungua hili shauri

Wakili Madeleka tusaidie kwenye kufungua hili shauri

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Wakili Madeleka popote ulipo, tunaomba uwasaidie Hawa wananchi wanaotapeliwa kwa kupitia jina la Ikulu. Nadhani wewe na Ex Mayor Bonny ndio mmebakia wenye uchungu na raia.

Kuna mtu anatumia jina la Ikulu, Waziri Mkuu na hata Jeshi letu la JWTZ kuwatapeli wananchi. Na mpaka sasa hivi kuna watu wamefilisika kutokana na tapeli huyu. Mwezi wa April mwaka huu RCO wa Temeke alifungua Jalada, ila baadae akatokomea gizani. Taarifa hizi zilishafika Hadi bungeni ila hakuna hatua iliyochukuliwa. Ni hatari Sana kwa taifa Kwa mtu kutumia majina ya Viongozi na hasa sehemu nyeti Kama Ikulu kutapeli raia wasio na kosa lolote.

Tulipeleka taarifa JWTZ wakakaa kimya, Bunge wakampiga kimya, ofisi ya Waziri Mkuu wakampiga kimya, ofisi ya Rais Zanzibar kwakapiga kimya. Sasa ni Bora hili jambo lifike mahakamani ili ukweli wote uwekwe wazi.

Madeleka na Mh Boni Yai popote mlipo tunaomba muwasaidie Hawa wananchi. Ni Bora taifa lielewe kinachoendelea hata Kama serikali itakaa kimya raia waendelee kuonewa.

Yeyote mwenye mawasiliano ya Wakili Madeleka anaweza kunipatia.
 
Kama vile kila mtu anajua nani katapeliwa nini na lini!?, umeishia kutaja ikulu, JWTZ, RCO etc, elezea nani anatumia jina la nani!?,katapeli nini kwa nani na lini!?.. unawahi wapi!?

Tafuta Uzi wa Jenerali Mwamwega nimeandika mengi Sana Toka mwezi February. Huwa nikirudia JF wanaufuta Uzi wangu.
 
Huu utapeli nimeuelezea kwa kina huko nyuma , Madeleka akikubali kuwasaidia nitampatia ushahidi wote , tumechoka na dhuruma. Polisi wanakula na matapeli wanaendelea kuwatishia raia na kuwabambikia kesi ambazo hazipo.
Ungeweka hiyo link tupate background ya malalamiko yako kama uwezi rudia kuandika upya utapeli wenyewe unaopelekea watu kufilisika.
 
Umeelewa kama vile wote tunaelewa tukio lilivyo.
Ujasiri wa kuficha wahalifu nalo nitatizo..funguka mkuu
 
Ungeweka hiyo link tupate background ya malalamiko yako kama uwezi rudia kuandika upya utapeli wenyewe unaopelekea watu kufilisika.

Acha kunisanifu. Nimeandika nyuzi karibia kumi kuhusu huu utapeli. Kama kweli hunisanifu search Generali Mwamwega zitakuja nyuzi nyingi.
 
Hivi madeleka kuna kesi yoyote aliwahi kushinda mahakamani?
 
Umeelewa kama vile wote tunaelewa tukio lilivyo.
Ujasiri wa kuficha wahalifu nalo nitatizo..funguka mkuu

Dah! Aiseeh nyie ni wageni JF?. Ebu search Generali Mwamwega zitakuja nyuzi nyingi. Huu Uzi ni wa kuomba msaada wa Mh Madeleka na Ex Mayor
 
Hayo ni matokeo ya kupenda vya rahisi, unatapeliwa kiulaiini. Tuache kuwaamini wala rushwa na watumia vibaya mamlaka.
 
Huyo Generali Mwamwega akifika mahakamani ndio mwisho wa huu utapeli. Na baada ya kuona anafuatiliwa kaenda Airtel kufuta namba yake ili asiwe traced.
 
Alikutapeli nini ?

Mkuu unanichosha. Fuatilia nyuzi za Generali Mwamwega Toka mwezi wa pili mwaka huu, ndio upate picha nzima ili upunguze maswali ya kizushi.
 
Duuuh! mkuu ungeweka hapa nyuzi zitumike kama rejea ya malalamiko yako,mambo ya kusema tusechi unakua unazingua sana, huyo tapeli ataendele kuwatapeli tu kama mnamficha.
 
Hayo ni matokeo ya kupenda vya rahisi, unatapeliwa kiulaiini. Tuache kuwaamini wala rushwa na watumia vibaya mamlaka.

Wala hakuna Mtu alitaka Cha mteremko. Hawa jamaa wametengeza serikali yao. Wanaitumia kuibia watu. Wana Kamishna wa Ardhi, Wana mkuu wa majeshi, Wana Rais wao etc. Wanatumia kampuni kuwapata wahanga wao.
 
Duuuh! mkuu ungeweka hapa nyuzi zitumike kama rejea ya malalamiko yako,mambo ya kusema tusechi unakua unazingua sana, huyo tapeli ataendele kuwatapeli tu kama mnamficha.

Mimi ndio namficha?. Haya bwana. Mimi nimeomba msaada wa Madeleka na Mh Boni
 
Back
Top Bottom