Wakili Madeleka tusaidie kwenye kufungua hili shauri

Hawawezi kushughulikia hilo jambo maana halitawasaidia kwenda viral, mara nyingi hao jamaa huwa wanacheza na upepo kwa mambo ambayo yatawaongezea umaarufu mtaani hasa mambo yanayolenga kuikosoa Serikali au kuichafua na sio watatuzi wa masuala nyeti ya kijamii kama hayo uliyoyaelezea
 
Huyo Generali Mwamwega akifika mahakamani ndio mwisho wa huu utapeli. Na baada ya kuona anafuatiliwa kaenda Airtel kufuta namba yake ili asiwe traced.
Huyu ni Jenerali wa kweli kweli huko JWTZ, au ndio hivyo ni jina tu?

Hata hivyo; hapo chini ya mada hii kunapoonyeshwa mada zinazo fanana, hiyo ya Jenerali hata haiibuki!
 
Kwanini hajanyakwa?!

Mpaka Leo nashangaa. Jalada lake lilifungiliwa na RCO wa Mkoa wa kipolisi wa Temeke mwezi February ila mpaka Leo kimya, anzidi kutapeli watu. Nadhani anakula na wakubwa. Maana kwenye utapeli wake anatumia ofisi ya Kamishna wa Ardhi Dodoma, Ikulu Zanzibar, Waziri Mkuu, JWTZ maana anajiita Generali wa JWTZ baada ya kupandisha ngazi kutoka Luteni Generali.

Kama mtu anatumia jina la Jeshi na hakamatwi? Tena anajipa cheo Cha kulingana na CDF ila jeshi li.ekaa kimya, hapo Kuna kitu kimejificha.
 

Nimesikitika Sana. Sasa nani atasaidia. Maana mpaka bungeni tumepeleka ushahidi wakaishia kuwapigia simu matapeli.
 
Mkuu poleni.

Ungecopy link ya hizo nyuzi na kuweka hapa ili watu wajue mwanzo wa story kuliko hivi unabishana na wapenzi wasikilizaji.

Once again poleni.
 
Labda anazitekeleza zile 4R wa vitendo.
 
Ungeweka hiyo link tupate background ya malalamiko yako kama uwezi rudia kuandika upya utapeli wenyewe unaopelekea watu kufilisika.
 
Labda ni kweli anatumwa na Ikulu tutajuaje
 
Labda ni kweli anatumwa na Ikulu tutajuaje

Hata Mimi napata wasiwasi. Inakuaje Ikulu hata ikipewa taarifa inakaa kimya. Maana majamaa wanatumia Hadi sauti ya Rais Samiah kuiba.
 
Yani Ikulu, JWTZ, Waziri Mkuu, Rais Mwinyi wote wapo kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…