carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Wakili Maduhu William amesema amri ya Mahakama kuhusu upatikanaji wa mawasiliano na mteja wake, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imetekelezwa kikamilifu baada ya kuruhusiwa kukutana naye katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.
Katika taarifa yake iliyotolewa Oktoba 29, 2026, Wakili Maduhu amesema alitembelea gereza hilo kwa lengo la kujiridhisha kuhusu utekelezaji wa amri hiyo ya Mahakama na kuonana na mteja wake.
Amesema alifanya mazungumzo na Lissu kwa faragha kwa zaidi ya dakika 45, huku maafisa wa Magereza wakiwa nje ya eneo la mazungumzo bila kusikiliza mazungumzo yao, kama ilivyoamriwa na Mahakama.
============
Leo nimetembelea Gereza la Ukonga nikiwa na malengo makuu mawili.
1. Kujiridhisha kama amri ya Mahakama inatekelezwa au ni propaganda za Magereza tu.
2. Pili kuonana na Mteja wangu Mhe Tundu Lissu.
Kuhusu suala la Kwanza naomba kutoa taarifa kwamba amri ya Mahakama imetekelezwa kikamilifu kwani sijazuiwa kuonana na mteja wangu kama ilivyokuwa hapo awali, nimeonana naye na tumekuwa na mazungumzo kwa zaidi ya dakika 45.
Kuhusu suala la pili, kama nilivyosema hapo awali,, nimeonana na Mhe Lissu, tumekuwa na mazungumzo kwa faragha kama Mahakama ilivyoamua kwa zaidi ya dakika 45 huku maafisa wa Magereza wakiwa nje wanaona lakini hawakuwa wanasikiliza mazungunzo yetu.
Kuhusu suala la kusoma nyaraka nalo limetekelezwa kikamilifu.
Mhe Lissu yu mzima wa Afya na mwenye tabasamu kama ilivyo kawaida yake.
Imetolewa na:
Wakili Maduhu William
29. Oktoba 2026
Pia Soma:
Mahakama imesema kuzuiwa kwa mawakili kuonana na Lissu Gereza la Ukonga kulimnyima mtuhumiwa nafasi ya kujitetea kikamilifu