Wakili Medium Mwale ahukumiwa kwenda jela miaka 5 kwa kosa la utakatishaji fedha

Wakili Medium Mwale ahukumiwa kwenda jela miaka 5 kwa kosa la utakatishaji fedha

Jaji Issa Maige wa Mahakama Kuu Arusha, amemuhukumu wakili Medium Mwale kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh 200 milioni kutokana na kosa la utakatishaji fedha

Pia amemuhukumu kifungo cha miaka saba ambacho ameshakitumikia kutokana na makosa mengine.

Sep 25, 2018 Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyakyomya, akisaidiana na mawakili wenzake, alimsomea upya Wakili Mwale mashtaka 41 ya utakasaji fedha haramu, kula njama, kughushi na kujipatia mali iliyopatikana kwa njia ya uhalifu.

Alidai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2009 na 2011.

Habari zaidi, soma=>Wakili Mediam Mwale adaiwa kukutwa na TZS 18 bilioni haramu - JamiiForums
Wakili Mwale na wenzake wasomewa upya mashtaka baada ya kukaa mahabusu kwa miaka 7 - JamiiForums

Hivi hii ndo hukumu yake baada ya kumfunga miaka yote hiyo? Uonevu tu! Na yale magari ya Mamilioni pale Police mnamrudishia au? maana kuna gari mpywa pale za thamani ya zaidi ya 200m "YAMEOZEA PALE HUWEZI AMINI"
 
hivi wakuu neno utakatishaji fedha lina maana gani maan muda mrefu nimekuwa nikilisikia na watu wanachukuliwa atua au hili tendo limekaa vip kifedha
Ni hivi mosi ni kuingiza pesa iliyopatikana isivyo halali katika mfumo halali wa fedha/matumizi pia kuingiza fedha halali katika matumiz yasiyo halali, mfano fedha halili kuingiziwa katika mfumo wa kufadhili ugaidi, au maharamia wapate fedha kwa utekaji wao kisha kwa mbinu kadha wa kadha kutumia fedha hizo kufanya biashara halali, mfano kufungua maduka nk.hyo ndo tafsir nyepesi niijuayo ,Tchao,muuza nyanya
 
Mke wa meneja wa crdb alikuwa anauza mahindi ya kuchoma dar baada ya kutelekezwa na mumewe alipopewa milion 200 na wakili mwale..
Laana ya huyo mke ndiyo imewafikisha hapo
 
Sory boss

Kutakatisha fedha ...

Ni kuwa na fedha nyingi ambazo hujazipata kihalali then mtu anaenda kuzitumia kwa mambo halali anachange the value of money so as to avoid to be seen as a culprit

Mfano serikali ikikuta wewe paap una bilion moja may be na unajua fika haujazipata kihalali ili uonekane ni zako for realy unazipeleka may be kununua shamba la hekari nyingi

Sory mkuu mi sina dharau naishi kwa kumheahimu kila mtu humu ndani na ni kweli na elimu kubwa nilikua sidhan kama ungereact hivi na nlkua najua may be tu ni unaleta masihara mkuu

Zaid zaid tuendelee kuijenga nchi yetu ...
Ili kuepuka utakatishaji fedha ukipata fedha isiyo halali unatakiwa uitumieje?
 
Sory boss

Kutakatisha fedha ...

Ni kuwa na fedha nyingi ambazo hujazipata kihalali then mtu anaenda kuzitumia kwa mambo halali anachange the value of money so as to avoid to be seen as a culprit

Mfano serikali ikikuta wewe paap una bilion moja may be na unajua fika haujazipata kihalali ili uonekane ni zako for realy unazipeleka may be kununua shamba la hekari nyingi

Sory mkuu mi sina dharau naishi kwa kumheahimu kila mtu humu ndani na ni kweli na elimu kubwa nilikua sidhan kama ungereact hivi na nlkua najua may be tu ni unaleta masihara mkuu

Zaid zaid tuendelee kuijenga nchi yetu ...
mkuu nashukuru umenielewesha vyema
 
Bora washamkhuku maana hakuwa hata anapelekwa mahakamani.. Pole sana Wakili Medium Mwale.. pole mno.. sijui na akina Sioi na Harry Kitilya na shose Sinare wanaendelea je na kesi zao.......

Vumilieni bado kitambo kidogo giza sana jua asubuhi yakaribia
Wakome, washenzi sana, wengine utajiri wetu wameshikilia wajinga na warafu wengine.
 
Ni hivi mosi ni kuingiza pesa iliyopatikana isivyo halali katika mfumo halali wa fedha/matumizi pia kuingiza fedha halali katika matumiz yasiyo halali, mfano fedha halili kuingiziwa katika mfumo wa kufadhili ugaidi, au maharamia wapate fedha kwa utekaji wao kisha kwa mbinu kadha wa kadha kutumia fedha hizo kufanya biashara halali, mfano kufungua maduka nk.hyo ndo tafsir nyepesi niijuayo ,Tchao,muuza nyanya
asante mkuu nimekupata vzr
 
Back
Top Bottom