Wakili Medium Mwale ahukumiwa kwenda jela miaka 5 kwa kosa la utakatishaji fedha

Hii ni katisha pesa hata billioni 500, kamatwa kubali kosa.. lipa faini sijui nini kidunchu ya ulizokatisha.. unaachiwa.. si mtu anabaki na pesa zake kama zipo kule na hukooo kama yupo smati..

Ukiachiwa maisha yanaendelea na pesa zako nyingiiii.. si ndio hivyo au?

Na kama ni hivi hawachukui pesa hizo zisaidie maendeleo ya nchi au mali kufidia karibu zote au zote. naona watu wataendelea tu kufanya haya kama kawa.

Sheria zingine sijui zikoje nchini hapa.. nielewesheni wadau..

Mahakama ya mafisadi nayo kama ipo ya hewa.. nilitegemea mapaparazi wawe wanatupa habari moto moto ila hakuna kitu.. Mh. Magufuli ningependa kumsikia akiongelea hili tena.
 
Huyu mtu kateseka sana..! Kwasababu ya chuki za watu na wivu..!
Ndio maana baada ya miaka 5 ameamua mwenyewe yaishe.

Kakiri makosa ili asomewe hukumu then alipe fine maisha yaendelee.

200milion sio kitu
 
Hivi hii ndo hukumu yake baada ya kumfunga miaka yote hiyo? Uonevu tu! Na yale magari ya Mamilioni pale Police mnamrudishia au? maana kuna gari mpywa pale za thamani ya zaidi ya 200m "YAMEOZEA PALE HUWEZI AMINI"
Mwisho wa siku lazima maisha yaendelee japo hayako fair
 
Kesi ya kutakatisha, ukikubali kosa, ama umekutwa na hatia mali zote zilizosababisha ufikishwe mahakamani zinataifishwa.
Mara nyingi kesi hii huchomoki, maana mamlaka zinataka uthibitisho wa biashara uliyofanya pamoja kiasi cha kodi ulicholipa serikalini.
 
Anaendeleaje huyu wakili??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…