Wakili Msomi Boniface Mwabukusi; Rais mtarajiwa toka Busokelo

Wakili Msomi Boniface Mwabukusi; Rais mtarajiwa toka Busokelo

Tanzania ya sasa inahitaji watu kaliba ya wakili Boniface Mwabukusi, wanaume wa shoka, akiongea mijizi na mifisadi yote ya mali za Umma inatetemeka popote pale ilipo.
Mungu ambariki sana Rais wetu ajaye Mwabukusi,
Amina.
Nani katetemeka?
 
Kwa sapoti kiduchu qnayopata Mwabukusi, Sasa hivi atakata upepo na kutokomea huko Busokelo
Unajua mtu kama Mwabukusi anaonekana ni mzalendo na jasiri sana. Na taifa linahitaji kiongozi ambaye yeye mwenyewe alipende na kulithamini alione kama mali yake binafsi kwa kuwa na uchungu nalo.

Sasa ndg yetu Boniohace kaonyesha analithamini taifa bila kujali maslahi yake inaona hata matamshi yake yako thabiti na anamaanisha anachokiamini. Tufike hatua kama taifa tuangalie maslahi ya taifa tuachane na viongozi wenye nia ya kujilimbikizia ukwasi na kulinda makundi yao.

Anatakiwa mtu atakayekuwa hana makundi aende jumba jeusi bila michango ya watu binafsi ambao watakuwa wamewekeza kwa rais ili akiingia madarakani waanze kupata faida. Hili limeligharimu sana taifa na linaendelea kuligharimu.

Tunahitaji kuwa na Tiss imara na majeshi imara yenye maono tofauti na wanaojifikiria wao tu. Tunatakiwa tukumbuke kuwa hili taifa litaendelea kuwepo hata mpaka pale vizazi vilivyo/vinavyolitafuna taifa vitakapobaki historia. Hivyo ni muhimu sana rasilimali za taifa ziheshimiwe na kulindwa na si kugawanwa kama inavyofanyika sasa mara hiki kimeuzwa kwa watu fulani mara huyu ana maslahi binafsi katika jambo fulani.

Utajiri na umasikini vyote ni hali tu lazima ifike hatua tuheshimiane wote na tuvilinde vilivyopo ili itakapofika wakati virithishwe kwa vizazi na vizazi.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania na kuilinda.
 
Back
Top Bottom