It's non-sense kumuita wakili msomi, kwani mawakili wapo ambao hawajasoma?
All over the World sio hoja ya msingi, kama tunataka kuangalia hivyo basi mambo yote ya kijinga yanayofanyika huko kwa wenzetu nasisi utashauri tuyafanye?
Watalaamu wa sheria, kwani kuna mtu anafanya kazi za sheria na sio msomi wa mambo ya sheria?
Watu weusi tunapenda kujikweza sana huu ndio ukweli.
Mheshimiwa flani, mbona huko kwa wenzetu unakolilia husikii wakisema honorable President Obama au honorable President Donald Trump?
Utasikia US President Donald Trump
Sasa hapa kwetu sema waziri John bila kutaja muheshimiwa Waziri John.
Ujinga mtupu, tunakomalia vyeo vya kijinga kuliko kufanya mambo ya maana.
Uliwahi kusikia Nyerere akiitwa Muheshimiwa? Unadhani kwanini hakuwahi kuitwa muheshimiwa ilihali alikua rais?
Watanzania tuache mambo ya sifa za kijinga