Katika kuunda Timu yake ya kuhakikisha anazidi kubaki madarakani - Mh. Spika, Ndugu Job Ndugai amegundua tishio au threat (kwa kimombo) kubwa kwake ni Naibu wake.
Huyu bwana mambo mengi amekuwa akiyafanya kwa kutumia vitisho vitisho tu akiachana kabisa na ule utaratibu wa kidemokrasia wa Mtangulizi wake Marehemu, Msomi Wakili, Samweli Sitta.
Huyu anataka kuwaonesha watu kuwa wanasheria si lolote na si chochote. Kwa kuweka msisitizo huo ameanza kuwashambulia eti watu wanaotambulishwa kwa majina ya fani zao waache mara moja.
Hii ina maana hataki Naibu wake atangulize utambulisho wa fani au umahiri wake kwa sababu wakigombea pamoja USpika ni lazima hizo sifa za fani na umahiri zitampunguzia credit.
Waliokuwa karibu na Naibu Spika jana baada ya maneno ya Bosi wake wanadai alishangaa sana na lugha ya machoni alionekana kutoafiki aliyokuwa akiyaongea Bosi wake.
Siku hizi za karibuni Job Ndugai amekuwa akitumia sana ubabe kuongoza bungeni na kutamani kuongoza hata mihimili mingine ili aonekana ana nguvu kubwa ya kimaamuzi hapa nchini kwani baada ya kujihisi hataweza kugombea URais 2025 amepania agombee tena huo USpika.
Wabunge wengi wanamchora tu na kujifanya wanamuunga mkono lakini 2025 ni lazima aliwe kichwa na asipokuwa makini akajaribu kugombea basi changamoto ya kisaikolojia itamkumba na kumsababishia shinikizo la damu na kitachofuata mimi sijui.
Ninamshauri amwandae Naibu wake kushika 2025, hiyo ndiyo salama yake.
Tukiweka ushabiki pembeni,Mimi Ndugai simpendi kabisa,
Lakini alichoongea kina mantiki,
Swali kwanini mawakili hujitambulisha kama"wakili msomi fulani bin fulan"(learned friend),huu utamaduni ulitokea UK kwa maelezo ya Spika,je una maana yeyote katika kuonyesha weredi wa hao mawakili?
Je mtu asipotambulishwa kwa cheo Cha kielimu alichonacho,Kuna mfanya ujuzi wake upotee?au ni njia ya kuji boost tu,na kujionyesha upo tofauti na wengine?!
Maana hivi vyeo na title,zipo kwenye CV,na Kuna sehemu inabidi uzionyeshe ama kwenye usahili,au kutafuta tender kukuza profile ya kampuni yako,sasa Kuna haja gani ya kutumia hivyo vyeo kwenye public?ukisema mi ni wakili msomi,muhandisi,Dokta,muhasibu kwa watu wengi hawaoni chochote zaidi ya Swaga.
Wacha sifa zikufate,mfano Watu kama Diamond,Kiba,Dangote,Mzee Mengi,Bakheresa,Mo,Shabiby wakijatambulisha tu majina yao,watu wote watajua Hawa ni kina nani na wamefanya na wanafanya nini?
Sasa ukisema Mimi wakili msomi! Then ??!!!so what!!!?