Wakili Msomi Peter Kibatala alivyomkaanga mtoto wa IGP Mahita kwenye kesi ya Mbowe

Wakili Msomi Peter Kibatala alivyomkaanga mtoto wa IGP Mahita kwenye kesi ya Mbowe

Wakili msomi Peter Kibatala V/S Mtoto wa IGP Mahita.

KIBATALA: Inspekta Mahita nimekufuatilia wewe ndiye ulikuwa arresting Officer?

MAHITA: Sahihi.

KIBATALA: Kazi ya Kingai ilikuwa nini?

MAHITA: Alikua Mkuu wa Msafara.

KIBATALA: Mkuu wa msafara ni role gani kwenye arresting?

MAHITA: Kimya.

KIBATALA: Adamoo pale Bomang'ombe alikula Chakula gani?

MAHITA: Wote walikula.

KIBATALA: Sitaki kujua wote. Nakuuliza Adamoo alikula nini?

MAHITA: Alikula Nyama Choma na Mo Energy.

KIBATALA: Nani alilipia?

MAHITA: Afande Kingai.

KIBATALA: Kwahiyo polisi mlikamata gaidi mkamnunulia nyama choma na ndizi? Mkampa na Mo Energy ya kushushia?

MAHITA: Kimya

KIBATALA: Na wengine mlikula pia?

MAHITA: Ndio

KIBATALA: Nani alilipia vyakula vyenu?

MAHITA: Afande Kingai.

KIBATALA: Siku zote mlizokua Hotel Dar alilipia nani?

MAHITA: Afande Kingai.

KIBATALA: Umewahi kushiriki zoezi la Retirement za Pesa alizotumia Kingai?

MAHITA: Hapana.

KIBATALA: Umewahi kumkabidhi Afande Kingai risiti za matumizi yako ili aweze kufanya retirement?

MAHITA: Hapana.

KIBATALA: Kwahiyo Kingai alitumia pesa za umma bila kuzitolea maelezo wala ripoti.

MAHITA: Siwezi kumsemea.

KIBATALA: Je unafahamu kuwa katika PGO namba 236 (3)ix unapomkamata mtuhumiwa unapaswa ujitambulishe wewe binafsi?

JAJI: Mpatie PGO.

KIBATALA: Ngoja nimepelekee.

MAHITA: Mheshimiwa Jaji, Wakili Kibatala ananionyesha kitu kingine.

JAJI: Muonyeshe taratibu, mtakuwa mmeshamchanganya.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji ngoja nimsomee (ananza kusoma)

MAHITA (anapaza sauti): Mheshimiwa Jaji, Wakili Kibatala anasoma vitu tofauti.

JAJI: Shahidi hebu tulia. Unafikiri mimi sitasoma hiyo PGO?

KIBATALA: Je ulipomkamata Adamoo ulitamka maneno yaliyoandikwa kwenye PGO?

MAHITA: Hapana.

KIBATALA: PGO 236(3) sehemu ya 10 inataka urekodi jibu la Adamoo katika Notebook yako. Je ulifanya hivyo?

MAHITA: Mheshimiwa Jaji, Kibatala anaongea vitu tofauti na PGO, nataka kumsaidia kidogo.

JAJI: Hiyo siyo kazi yako.

KIBATALA: soma hapa kwenye PGO

MAHITA: (anasoma).

KIBATALA: je ni sahihi kuwa Misingi yote inayoainishwa katika PGO kuhusu ukamataji lazima ifuatwe kwa kunyooka kama RULA?

MAHITA: Ni sahihi.

KIBATALA: Unafahamu kuwa unakuja kutoa ushahidi kuhusu statement ya Dama Kasekwa?

MAHITA: Sifahamu.

KIBATALA: Okay. Sasa, mwambie Jaji kwamba hujui kama ulikuja kutoa ushahidi kwenye Kesi ndogo katika kesi ya msingi kuhusu Adamoo.

MAHITA: Hilo sifahamu.

KIBATALA: Kumbe tupo na shahidi ambaye hajui amekuja kufanya nini Mahakamani?

#WakiliWaJamhuri: Objection Mheshimiwa Jaji. Tunaomba maswali ya Kibatala yazingatie utu na kuacha udhalilishaji.

JAJI: Naomba tuzingatie utu.

KIBATALA: Naomba unisomee hapa katika PGO kuhusu Notebook.

MAHITA: Nadhani tafsiri ya PGO hainilazimishi kukumbuka kila kitu Mahakamani.

KIBATALA: Sihitaji tafsiri yako, nimekwambia soma.

MAHITA: Anashindwa kusoma.

Jaji anaingilia kati na kusema "naona Mmechoka, natoa mapumziko tutarudi baada ya nusu saa"

Malisa GJ

View attachment 1942769
Magaidi wananunuliwa mbuzi Choma na Mo energy ya kushushia.😀😀😀😀
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] #WakiliWaJamhuri: Objection Mheshimiwa Jaji. Tunaomba maswali ya Kibatala yazingatie utu na kuacha udhalilishaji.
Hawa wanajidhalilisha wenyewe waache wadhalilike.

Katika hali ya kawaida tu Jaji ameshaelewa ukweli kwamba hapa ni kanjanja tupu, kesi kama hii kwenye nchi zilinyooka haipaswi kupotezea watu muda ni Jaji kuwafukuza Polisi mahakamani na kuwaonya mahakama si chombo cha kuja kuigizia filamu.
 
Hawajarudi tu mahakamani waendelee kutujuvya?

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 #WakiliWaJamhuri: Objection Mheshimiwa Jaji. Tunaomba maswali ya Kibatala yazingatie utu na kuacha udhalilishaji.
Mwisho wa ubaya ni aibu.

Hilo ndilo tatizo kubwa la kesi za kubambika, Polisi hakumbuki tena kuwa yeye ni mtumishi wa Umma, ambapo anatakiwa afanye kazi kwa kufuata sheria na kanuni.

Katika kesi ya Mbowe, mapolisi hata hizo Police General Orders zao hawakutaka kuzifuata😁
 
Ninacheka mno. Yaani hii ni aibu na fedheha kwa nchi. Mh. Rais usikubali kubebeshwa hili igizo lililobuniwa enzi za yule Lucifer, the dictator. Sasa wameliamsha ili kukuchafua. Rais wangu umezingukwa na bàadhi ya watendaji wenye agenda zao dhidhi yako. Ifike mahali uteue wote muhimu vinginevyo unaharibiwa.
 
DPP kwa kuficha hii aibu wangemaliza kwa kuifuta kesi kama hizo za kina Ruge watoe sababu yeyote tutawaelewa kuliko kila siku watu wanajibu maswali kama watoto wa chekechea...kuulizwa maswali na Kina Kibatala ni sawa na kushindana Control na Gaucho hata Jaji atakua upande wa Gaucho...
 
Hawa wanajidhalilisha wenyewe waache wadhalilike.

Katika hali ya kawaida tu Jaji ameshaelewa ukweli kwamba hapa ni kanjanja tupu, kesi kama hii kwenye nchi zilinyooka haipaswi kupotezea watu muda ni Jaji kuwafukuza Polisi mahakamani na kuwaonya mahakama si chombo cha kuja kuigizia filamu.
Kesi ya Zuma polisi walijichelewewsha muda wa kuingia mahakamani Jaji aliwapa onyo wakifanya siku ingine hivyo wataenda ndani..bongo polisi wanaanzisha sheria zao eti simu marufuku na wanaendelea kujadili Jaji anawasikiliza watu wasiojua kitu...
 
MAHITA (anapaza sauti): Mheshimiwa Jaji, Wakili Kibatala anasoma vitu tofauti.

JAJI: Shahidi hebu tulia. Unafikiri mimi sitasoma hiyo PGO?
Hahaaahaa kapiga kelele utadhani kabanwa naniliu hahahhaha Jaji nae kammaliza

Hii imenikumbusha tukiwa wadogo jamaa walikuwa wanapigana!

Mmoja wao kwa sauti kubwa akapiga kelele akisema;
Anang'ataaa,anang'ataaa😆😆
 
Ninacheka mno. Yaani hii ni aibu na fedheha kwa nchi. Mh. Rais usikubali kubebeshwa hili igizo lililobuniwa enzi za yule Lucifer, the dictator. Sasa wameliamsha ili kukuchafua. Rais wangu umezingukwa na bàadhi ya watendaji wenye agenda zao dhidhi yako. Ifike mahali uteue wote muhimu vinginevyo unaharibiwa.
Nina imani Mama anayajuwa yoote hayo uliyoyasema na hata sisi kina kaj.....nani tunayajuwa.Kwa uwezo wa Mwenyezimungu wale wenye nia ovu na Mama watashindwa.
 
Back
Top Bottom