Wakili Musa Kwikima (1939 – 2020) Katibu Tume ya Waislam ya Mgogoro wa EAMWS, 1968

Wakili Musa Kwikima (1939 – 2020) Katibu Tume ya Waislam ya Mgogoro wa EAMWS, 1968

Mungu amlaze mahala pema peponi hawa wasio amini wakisikia tu majina ya hawa wazee chuki zao hushindwa kuzificha dhahiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Madi...
Lakini hii ndiyo historia ya Tanganyika hatuwezi kuibadilisha.

Wamejaribu watu kuibadili na natokeo yake ndiyo haya tunayaona leo baada ya kuandikwa historia ya kweli.

Katika kujaribu kutengeneza lili lililoharibika ndiyo wasomi wa nchi hii wakaamua kukaa kitako na kuandika historia ya Mwalimu Nyerere kuanzia kuzaliwa kwake hadi anafika Dar es Salaam katika kitovu cha siasa za ukombozi.

Walipofika hapa Mwalimu kaja Dar es Salaam wakaja kufanya mahojiano nami na niliwapa Nyaraka za Sykes na picha za zamani za Mwalimu za wakati ule vilevile baadhi ya picha hizo kutoka katika kumbukumbu za akina Sykes kama nilivyozitumia katika kuandika kitabu cha Abdu Sykes.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madi...
Lakini hii ndiyo historia ya Tanganyika hatuwezi kuibadilisha.

Wamejaribu watu kuibadili na natokeo yake ndiyo haya tunayaona leo baada ya kuandikwa historia ya kweli.

Katika kujaribu kutengeneza lili lililoharibika ndiyo wasomi wa nchi hii wakaamua kukaa kitako na kuandika historia ya Mwalimu Nyerere kuanzia kuzaliwa kwake hadi anafika Dar es Salaam katika kitovu cha siasa za ukombozi.

Walipofika hapa Mwalimu kaja Dar es Salaam wakaja kufanya mahojiano nami na niliwapa Nyaraka za Sykes na picha za zamani za Mwalimu za wakati ule vilevile baadhi ya picha hizo kutoka katika kumbukumbu za akina Sykes kama nilivyozitumia katika kuandika kitabu cha Abdu Sykes.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu akujaalie maisha marefu yenye fanaka uzidi kutudadafulia mengi tusiyo yajua juu hawa wazeee wetu japo wasio amin wanachukia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAKILI MUSA KWIKIMA (1939 – 2020)
KATIBU TUME YA WAISLAM YA MGOGORO WA EAMWS, 1968

Unaanzaje kuandika historia ya mtu kama Musa Kwikima katika Mgogoro wa EAMWS?
Unaanzaje?

Historia ya Musa Kwikima ni historia ya Waislam baada ya uhuru mwaka wa 1961 walipokuwa wakipambana na changamoto mpya baada ya ile ya changamoto ya ukoloni wa Waingereza. Changamoto ya ukoloni wa Muingereza Waislam waliikabili vizuri wao wakiwa mstari wa mbele wakipanga mikakati ya kila aina kuhakikisha kuwa ukoloni unatokomezwa na kwa hakika ulitokomezwa. Nusu karne imepita hakuna anaejua historia ya wazalendo hawa. Wenye madaraka na elimu ya kuitafiti historia hii wanaiogopa.

Unaanzaje kuandika taazia ya mtu kama Musa Kwikima na historia yake kama mwanasheria kijana, Jaji ya Mahakama Kuu na mmoja katika wazalendo waliopigana kutetea haki za Waislam baada ya uhuru?

Wakati wa Musa Kwikima ulikuwa wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ulikuwa pia ni wakati wa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir mufti wa Tanganyika kiongozi wa juu wa Waislam aliyempokea Nyerere na waongoza Waislam katika umoja wa wananchi kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wakati wa Musa Kwikima ulikuwa wakati wa Abeid Amani Karume Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Tanzania.

Wakati wa Musa Kwikima ulikuwa wakati wa Said Ali Mswanya, Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati wake ulikuwa wakati wa Hamza Aziz, Inspector General of Police (IGP).

Wakati wa Musa Kwikima ulikuwa wakati wa Sheikh Abdallah Chaurembo na Sheikh Kassim Juma wote wanazuoni wanafunzi wakipiga goti katika darsa za Sheikh Hassan bin Ameir.

Wakati wa Musa Kwikima ulikuwa wakati wa Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed tayari wameshapoteza nafasi zao za uongozi katika serikali na TANU, Tewa akabakia kuwa Rais wa EAMWS upande wa Tanzania Makamu Mwenyekiti wake akiwa Bi. Titi Mohamed.

Pamoja na viongozi hawa walikuwapo pia Suleiman Kitundu na Rajab Diwani wajumbe wa Kamati Kuu ya TANU waliokuwa sikio analosikizia Mwalimu Nyerere.

Hawa wote niliowataja wanahusika kwa namna moja au nyingine na historia ya Musa Kwikima. Historia ya Musa Kwikika haikamiliki bila ya kuwataja watu hawa.

Lakini ukipenda unaweza ukawaongeza watu hawa wengine – Bilal Rehani Waikela muasisi wa TANU Tabora na Katibu wa EAMWS, Rashid Kayugwa na Geofrey Sawayya.

Hawa wawili wa mwisho walikuwa watumishi katika vyombo vya Usalama vile vya siri na vya dhahir.

Unaweza pia ukawaongeza Benjamin Mkapa Mhariri wa gazeti la TANU The Nationalist na Martin Kiama Mkurugenzi wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Kati ya mwaka wa 1963 hadi kufikia mgogoro wa EAMWS mwaka wa 1968 yalitokea mengi.

Mwaka wa 1963 Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mzee Iddi Tulio lilivunjwa kwa tuhuma za ‘’kuchanganya dini na siasa,’’ tuhuma iliyopekea Mweyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee afukuzwe TANU mwaka wa 1958.

Mwaka wa 1964 masheikh wengi waliwekwa kizuizini kufuatia maasi ya wanajeshi.

Mwaka wa 1965 katika Uchaguzi Mkuu, Tewa Said Tewa na Titi Mohamed walishindwa katika kura za Ubunge, Tewa Kisarawe na Bi. Titi Rufiji.

Yote haya yalimpita kijana Musa Kwikima kama mambo ya kawaida. Hakujua kuwa zote zile zilikuwa ishara ya jambo kubwa na zito litakalomalizikia kwa kuvunjika EAMWS na kusimamisha si ujenzi wa EAMWS peke yake bali na mipango yote iliyokuwa ikiendelea ya kujenga shule athari ambayo hadi leo inaonekana.

Kijana mdogo Musa Kwikima alyaona yale tu yaliyokuwa hadhir mbele ya macho yake.

Musa Kwikikima wala katika fikra zake haikumpitikia kuwa haya yaliyokuwa yakitokea yeye hayajui, yote yalikuwa yanatengeneza jukwaa kubwa ambalo yeye atakujakuwa mmoja wa waigizaji wa mchezo uliokuwa unatayarishwa baina ya wanasiasa ndani ya TANU na serikali na viongozi wa EAMWS ikiongozwa na Sheikh Hassan bin Ameir na Tewa Said Tewa na Waislam kwa ujumla wao wakiwa watazamaji.

Waislam kwa hakika walikuwa kama watazamaji kwani mchezo ulipokuwa unachezwa kwenye jukwaa hawakushangilia wala hawakuonyesha kuwa mchezo ule haukuwa na mvuto wowote.

Ilikuwa kama vile hawajui nini kinatendeka, nini wanatakiwa kufanya na nini hatima ya mchezo ule.

Mgogoro wa EAMWS ulianza mara tu baada ya Mwalimu Nyerere kuweka jiwe la msingi tayari kwa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Waislam kilichokuwa kinajengwa na EAMWS.

Hii ilikuwa miezi migumu sana kwa Musa Kwikima na kwa Waislam.

Asubuhi akiamka Musa Kwikima atasikiliza tarifa ya habari ya RTD na baada ya hapo atasoma The Nationalist habari kuu katika vyombo vyote hivyo ikiwa ni Mgogoro wa EAMWS. Wakati wa mgogoro huu Musa Kwikima alikuwa bado kijana mdogo wa miaka 29 ndiyo kwanza kamaliza Chuo Kikuu kama Mwanasheria.

Mgogoro huu ulimkuta Musa Kwikima katika ndoto za ujana na matumaini makubwa katika maisha yake ya kulitumikia taifa lake changa la Tanzania kama mwanasheria. Musa Kwikima alikuwa mmoja wa wanafunzi wasiozidi 10 waliohitimu katika kundi la kwanza katika Idara ya Sheria Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Mtaa wa Lumumba.

Tatizo la EAMWS lilianza mara tu baada ya uhuru ndani ya Halmashauri Kuu ya TANU mwaka wa 1963 Nyerere alipopambana na Bi. Titi katika mjadala ulioletwa na Selemani Kitundu na Rajab Diwani kuhusu nafasi ya Aga Khan Tanganyika kama Patron wa EAMWS.

Baadae mwaka huo 1963 katika mkutano wa EAMWS uliofanyika Dar es Salaam lilijitokeza kundi dogo ndani ya EAMWS kikidai Tanganyika ijitoe katika umoja ule ili iundwe jumuia mpya.

Mzee Waikela anasema fikra hizi hazikuwa fikra za Waislam bali zilikuwa fikra zilizopandikizwa kutoka nje ya umma. Sheikh Hassan bin Ameir aliwatahadharisha baadhi ya viongozi wa EAMWS kuwa makini na wawe tayari kupambana na kikundi hiki.

Hoja hii ilipoletwa katika ule mkutano ilipingwa na msemaji mkuu alikuwa Bilal Waikela na alieleza chanzo cha fikra ile. Inasemekana serikali haikuwa inaiangalia EAMWS kwa jicho jema na katika kutaka kukata mzizi wa fitna na kuliweka jambo lile wazi iliamuliwa kuwa Rais Julius Nyerere aalikwe kufunga mkutano ule na asomewe risala maalum aelezwe msimamo wa Waislam wa Tanganyika kuhusu EAMWS.

Waikela alimsomea Nyerere risala kali sana kwanza akieleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika, kheri angeishia hapo.

Waikela wakati ule kijana wa miaka kiasi ya 30 akahitimisha risala ile kwa kutoa onyo kuwa Waislam wasichokozwe wakaja kuwasha moto ambao hakuna atakaeweza kuuzima.

Yapata zaidi ya miaka 20 iliyopita Musa Kwikima alinipigia simu wakati ule niko Tanga akinieleza nia yake ya kuandika historia mgogoro wa EAMWS.

Mimi nilimuhimiza kuandika kwani niliamini Musa Kwikima atakuwa na mengi ya kueleza kwani yeye ndiye alikuwa katibu wa Tume ya Kuchunguza Mgogoro wa EAMWS.

Nimeisoma Taarifa ya Musa Kwikima ambayo aliitoa kwa ‘’Waislam Wote,’’ pamoja na Taarifa ya Fedha. Nilijua lau kama ni miaka mingi imekwishapita lakini yatakuwapo mengi ya Waislam kujifunza katika historia yao.

Ikawa katika kipindi cha takriban miaka 20 iliyopita kila tukikutana au kuzungumza kwenye simu yeye akiwa Tabora mimi niko Tanga lazima tutazungumza kuhusu mswada wa kitabu chake hiki. Mara ya mwisho kuzungumza na Musa Kwikima ilikuwa majuma mawili yaliyopita alipokuja kunitembelea nyumbani kwangu akiwa kafuatana na mwanae Karama Musa Kwikima.

Ilkuwa muda mfupi baada ya Mwalimu Nyerere kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu Cha Waislam, Chang’ombe huku akiangaliwa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Tewa Said Tewa, siku moja RTD ikatangaza kuwa Bukoba inajitoa katika EAMWS.

Hili lilikuwa jambo la kushtusha.
Haikufika hata juma moja, Tanga nayo ikatangaza kujitoa katika EAMWS.

Rais wa EAMWS Tewa Said Tewa akaitisha mkutano Dar es Salaam wa viongozi wa EAMWS kutoka mikoa yote ya Tanzania kuja kujadili hali ile.

Kilichomtisha Tewa Said Tewa ilikuwa nguvu ya vyombo vya habari RTD chini ya Martin Kiama na The Nationalist chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa ulivyokuwa unatangaza mgogoro ule. Habari zilizokuwa zinatolewa zilikuwa ni zile za kundi lililojitenga na zikiandikwa namna ya pekee. RTD na The Nationalist halikutoa nafasi kwa viongozi wa EAMWS kujieleza.

Mkutano wa EAMWS uliuda tume na hapa ndipo alipoingia Musa Kwikima kijana wakati ule Jaji wa Mahakama Kuu kwa kuombwa atiwe katika Tume ya Uchunguzi wa Mgogoro wa EAMWS iliyokuwa na wajumbe saba.

Musa Kwikima akawa Katibu wa tume hii. Wakati huo tayari mikoa 9 ilikuwa tayari imeshajitenga na EAMWS kati ya mikoa 17 iliyokuwapo. RTD na The Nationalist vikawa tayari vimejenga mgogoro ule kufikia hali ya kuonekana kuwa ni mgogoro mkubwa sana Waislam wanawakataa viongozi wabovu na wapinga serikali ndani ya EAMWS.

Hivi ndivyo Musa Kwikima alivyotumbukia katika kapu ambalo propaganda ilijenga kuwa ni kapu lililokuwa na samaki waliochina.
Ndani ya kapu lile alikuwamo Sheikh Hassan bin Ameir, Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed.

Hakuna ambae alikuwa hajui historia za watu hawa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katikati ya mgogoro huu uliokuwa umewatia simanzi watu wa Dar es Salaam mwezi huo wa Oktoba, 1968 Abdulwahid Sykes akafariki dunia.

Msiba wa Abdul Sykes uliwarejeshea watu wa Dar es Salam kumbukumbu nyingi za Nyerere alipoingia mjini na kupokelewa na Abdul Sykes wakikumbuka kumuona akiongozananae wakati mwingine wakitembea kwa miguu pamoja mitaa ya Gerezani, Abdul akimtambulisha Nyerere katika juhudi za kuijenga TANU.

Ule ndiyo ulikuwa wakati TANU inanyanyukia kwa nguvu na watu wa Dar es Salaam walikiunga mkono chama kwa hali na mali.

Lakini miezi ile mitatu ya mwisho ya mwaka wa 1968 mji ulikuwa umegubikwa na hofu.
Masheikh wengi kipindi hiki walikuwa wakigongewa milango usiku wa manane na kukamatwa. Hakika huu ulikuwa wakati mgumu.

Kimetokea nini ndani ya EAMWS kiasi cha kukumbwa na haya yote?

Waislam walijiuliza kwa mshangao vipi juzi Nyerere kaweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu cha Waislam chini ya usimamizi wa EAMWS leo ghafla viongozi wake kutoka mikoani wanatokea katika magazeti na kusikika katika radio wakisema hawana haja nayo?

Hili halikuwa jambo rahisi kueleweka.

Waikela alikuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya Kikwima na hakuchelewa alimwonya kijana wake akamwambia, ‘’Musa hili jambo litakuharibia kazi yako.’’

Nini likukuwa jibu la Musa Kwikima?

‘’Kazi hii ni ya Allah lazima niifanye kutafuta salama ya dini yangu ikiwa ndiyo itakuwa mwisho wa kazi yangu basi hivi ndivyo Allah alivyoniandikia.’’

Musa Kwikima alikuwa kijana mdogo wa miaka 29.

Waikela baada ya ule mkutano wa mwaka wa 1963 ambao alimsomea Nyerere ile risala kali, mwaka uliofuatia baada ya maasi ya wanajeshi Januari 1964 alitiwa kizuizini na kufungwa jela ya Uyui huko kwao Tabora.

Waikela alikuwa anajua mengi sana katika mgogoro ule na nini kilikuwa kinatafutwa.

Tatizo lilikuwa kwa Waislam kujenga Chuo Kikuu.
Inawezekana Musa Kwikima hakuwa anayajua mengi katika mgogoro ule hadi hapo baadae kabisa.

Kwikima hakujua kuwa kulikuwa na moto wa makumbi unafukuta chini kwa chini kuanzia mwaka wa 1963 baada ya Muslim Congress mbili ya mwaka wa 1962 na 1963 mikutano ambayo ilikuja na mipango yake ya elimu kwa Waislam mipango iliyopelekea ujenzi wa Chuo Kikuu.

Mwezi Novemba ile Tume ya Kwikima ilikwenda kuonana na Waziri wa Habari Hasnu Makame ofisini kwake kumtaka azuie propaganda za RTD na The Nationalist dhidi ya viongozi wa EAMWS.

Hapakutokea mabadiliko yoyote.

Sauti zilizokuwa zikisikika zilikuwa zile zile za wapinzani waliojitenga na EAMWS. Hapo ndipo Tewa Said Tewa na Bi. Titi Mohamed wakaamua kwenda kuonana na Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani.

Yale waliyoyasikia kutoka kinywani kwa Nyerere hayakuhitaji mkalimani kuyaeleza.

Kama Nyerere alitoka kichwa chini katika mkutano wa EAMWS baada ya kusomewa risala na Bilal Waikela safari hii ilikuwa zamu ya Tewa na Bi. Titi kuondoka nyumbani kwa Nyerere, Msasani vichwa vyao wameinamisha.

Iliwadhihirikia wazi kuwa Nyerere hakuitaka EAMWS katika nchi yake.

Mwezi Desemba kundi lililojitenga likafanya mkutano wao wa kwanza Ukumbi wa Arnautoglo agenda ikiwa kujadili mgogoro wa EAMWS.

Baada ya mkutano huu haukupita muda wakatangaza kuitisha mkutano mwingine Iringa uliopewa jina kuwa ni ‘’Mkutano wa Waislam wa Tanzania.’’

Ilikuwa wazi kuwa mkutano huu wa Iringa ulikuwa na nia ya kuishawishi serikali kuivunja EAMWS na kuunda chama mbadala.

Tume ya Kwikima nayo ikatoa taarifa yake kwa Waislam tarehe 11 Desemba 1968 na ikatangaza kuitisha Mkutano Mkuu wa EAMWS mwezi unaofuatia Januari 1969. Musa Kwikima alikuwa sasa anakimbilia kutimiza miaka 30 kwani alikuwa amezaliwa tarehe 19 Machi, 1939.

Kwa miezi mitatu mfululizo Musa Kwikima hakuwa na uwanja ambao angeweza kueleza chochote katika ule mgogoro na sababu ilikuwa vyombo vyote vilikuwa kama vile vimewekwa makhsusi kutumikia wale wapinzani wa EAMWS.

Taarifa ya Musa Kwikima ilileta matumaini mapya kwa Waislam kuwa labda Tume ya Kwikim sasa itamaliza mgogoro ule na ujenzi wa Chuo Kikuu utaendelea baada ya kutekelezwa kwa mapendekezo ya Tume.

Mategemeo yao makubwa Waislam yalikuwa kwa Sheikh Hassa bin Ameir kwani wapinzani wa EAMWS hawakuwa na kiongozi mwenye hadhi ya Sheikh Hassan bin Ameir.

Aliyoyafanya Sheikh Hassan bin Ameir katika dini na ndani ya TANU yalikuwa hayana mfano wake.

Sheikh Hassan bin Ameir akawa ni kizingiti kikubwa kwa wale waliotaka kufanya mkutano Iringa.
Amri ikatoka kuwa Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe.

Kazi ya kukamata ni kazi ya Jeshi la Polisi. Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya alipompa amri IGP Hamza Aziz kumkamata Sheikh Hassan bin Ameir, Hamza Aziz aliuliza kosa alilofanya Sheikh Hassan bin Ameir.

Jibu alilopewa ni kuwa Sheikh Hassan alikuwa anataka kupindua serikali.

Hamza Aziz alijibu kuwa huo ni uongo na akakataa kutii amri ile.
Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Usalama wa Taifa wakamkamata Sheikh Hassan bin Ameir usiku nyumbani kwake Magomeni na usiku ule ule akasafirishwa kwao Zanzibar na kuambiwa kuwa asirejee bara maisha yake yote.

Kizingiti kikawa kimeondolewa.
Mkutano uliokusudiwa kufanyika Iringa ukafanywa na ulifunguliwa na Abeid Amani Karume tarehe 13 Desemba 1968.

Mkutano huu ukapitisha katiba ya mpya ya jumuiya ya Kiislam iliyopewa jina la BAKWATA katiba hii ilikuwa sawasawa na katiba ya TANU.

Historia ikawa kama vile imejirudia.
TANU ilinakili katiba yake neno kutoka katiba ya Convetion People’s Party (CPP) ya Kwame Nkrumah.

BAKWATA ikaomba itambuliwe na serikali na ipige marufuku EAMWS.
Bila kuchelewa Musa Kwikima alitoa taarifa ya EAMWS kuhusu BAKWATA.

Kwikima baada ya siku hii mwaka wa 1968 hakupata tena kuandika maneno ya ukweli kama hayo hao chini hadi anafariki.

Kwikima alisema:

‘’Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsi hata ikiwa mikoa yote 17 ikijitoa haitamaananisha kuwa jumuiya imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.’’

Musa Kwikima kabla ya mgogoro wa EAMWS alikuwa ameteuliwa na Rais Nyerere kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwikima ndiye hasa alikuwa nguvu kuu katika Tume ya Waislam ya kunusuru EAMWS.

Baada ya kuundwa kwa BAKWATA Musa Kwikima alihamishwa kutoka Dar es Salaam na kupelekwa Mwanza kama Hakimu Mkazi na Rais Nyerere akamvua madaraka ya Ujaji.

Laiti angelibakia kama Jaji Musa Kwikima ndiye angelikuwa Jaji Mkuu wa kwanza mzalendo baada ya kuondoka Philip Telford Georges kutoka Dominica.

Huyu ndiye ndugu yetu Musa Hussein Almasi Kwikima.

Tunamuomba Allah amsamehe madhambi yake na alifanye kaburi lake kuwa moja ya mabustani ya peponi.
Amin

PICHA: Kulia ni Musa Kwikima, Mohamed Chande (Jaji Mkuu Mstaafu) na Siraji Musa Kwikima.
View attachment 1433505
Mimi niliyepata kumsikia jaji Musa kwenye baraza maarufu Kigoma meza ya duara, miaka miwili iliyopita, alieleza mengi zaidi ya haya. Mengine yanatisha. Nae alipata kusema angeendelea kuhudumu angekuwa jaji mkuu. Umeeleza sahihi japo hujamaliza yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliyepata kumsikia jaji Musa kwenye baraza maarufu Kigoma meza ya duara, miaka miwili iliyopita, alieleza mengi zaidi ya haya. Mengine yanatisha. Nae alipata kusema angeendelea kuhudumu angekuwa jaji mkuu. Umeeleza sahihi japo hujamaliza yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngali...
Ungeeleza ulichosikia kutoka kwake sote tungenufaika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliyepata kumsikia jaji Musa kwenye baraza maarufu Kigoma meza ya duara, miaka miwili iliyopita, alieleza mengi zaidi ya haya. Mengine yanatisha. Nae alipata kusema angeendelea kuhudumu angekuwa jaji mkuu. Umeeleza sahihi japo hujamaliza yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi alijuaje kama angekuwa jaji mkuu wote tunajua jaji mkuu huteuliwa na rais ni vigezo gani alifikiri yeye anavyo na wengine hawakuwa navyo
 
Mashaaah Mzee katika vitu ambavyo tunapindishwa nchini humu ni historia ya Tanganyika imefinywa sana Jazakhallah Ntakitafuta kitabu chako sheikh
 
Nafikiri utakubaliana na mimi linapokuja swala la uteuzi inategemeana na mapenzi ya anayeteua ndio maana wakati mwingine tunaona wako waliostahili kuteuliwa lakini hawateuliwi
Rod. ..
Umesema kweli lakini hiki ni kisa kingine kabisa kinaanza na mgogoro ukiokuwapo ndani ya TANU kati ya Nyerere na baadhi ya waliokuwa washirika wake wakati wa kupigania uhuru ukaishia kwa serikali kuivunja EAMWS na taasisi zingine kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Ukiujua undani wa mgogoro huu na nafasi ya Mussa Kwikima utaelewa kwa nini alikosa nafasi ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rod. ..
Umesema kweli lakini hiki ni kisa kingine kabisa kinaanza na mgogoro ukiokuwapo ndani ya TANU kati ya Nyerere na baadhi ya waliokuwa washirika wake wakati wa kupigania uhuru ukaishia kwa serikali kuivunja EAMWS na taasisi zingine kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Ukiujua undani wa mgogoro huu na nafasi ya Mussa Kwikima utaelewa kwa nini alikosa nafasi ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi siko kwenye mgogoro nishawahi kukutana na marehemu akidai alipaswa kuteuliwa kuwa jaji mkuu nisichokubaliana naye yeye sio anayefanya teuzi Haruni Mahundi aliteuliwa kuwa mkui wa polisi wakati kulikuwa na mapolisi wengi wamemzidi vyeo sifa ya elimu lakini yeye akawapiku kwenye teuzi kuna vitu vingi wanaangalia sio usomi peke yake
 
Mimi siko kwenye mgogoro nishawahi kukutana na marehemu akidai alipaswa kuteuliwa kuwa jaji mkuu nisichokubaliana naye yeye sio anayefanya teuzi Haruni Mahundi aliteuliwa kuwa mkui wa polisi wakati kulikuwa na mapolisi wengi wamemzidi vyeo sifa ya elimu lakini yeye akawapiku kwenye teuzi kuna vitu vingi wanaangalia sio usomi peke yake
Rod. ..
Siwezi kukulazimisha.

Mimi nimeandika historia yote kwa utafiti na iko paper, "Islam and Politics in Tanzania," (1989).

Paper hii inakamilisha sehemu ya mwisho ya kitabu changu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," London 1998.

Kuamini au kutoamini kitu ni khiyari ya mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijapinga historia wala utafiti kwa sababu mpaka umeileta hapa ni wazi umetumia muda mrefu na kuongea na watu mbalimbali na hata swali nalohoji sio maneno yako bali yametoka kwa mhusika nisichokubaliana naye ni hoja ya yeye kuteuliwa kuwa jaji mkuu labda kama teuzi angekuwa anafanya yeye binafsi
 
Mimi sijapinga historia wala utafiti kwa sababu mpaka umeileta hapa ni wazi umetumia muda mrefu na kuongea na watu mbalimbali na hata swali nalohoji sio maneno yako bali yametoka kwa mhusika nisichokubaliana naye ni hoja ya yeye kuteuliwa kuwa jaji mkuu labda kama teuzi angekuwa anafanya yeye binafsi
Rod...
Nami ninachueleza ni kuwa kama si mgogoro ule Mussa Kwikima angepata ile kazi na Sheikh Hassan bin Ameir asingekamatwa na kufukuzwa Tanganyika na BAKWATA isingekuwapo na mambo chungu nzima yangekuwa tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi alijuaje kama angekuwa jaji mkuu wote tunajua jaji mkuu huteuliwa na rais ni vigezo gani alifikiri yeye anavyo na wengine hawakuwa navyo
Suala la alijuaje au alifikiri ni masuala ya dhana, kiukweli watu kama kina barnabas sammata, Joseph warioba au butiku wengeweza kukusaidia gonjwa lako la chuki lakini zaidi ni kuwa huyu bwana (Mungu Amlaze mahala pema) Aliitumikia nchi kwa uzalendo wake wote ndio ukaona hata akateuliwa mara mbili kuwa Jaji, hizi habari maskini angepaswa kuziandika kuondoa mkanganganyiko kwa hawa wajinga
 
Suala la alijuaje au alifikiri ni masuala ya dhana, kiukweli watu kama kina barnabas sammata, Joseph warioba au butiku wengeweza kukusaidia gonjwa lako la chuki lakini zaidi ni kuwa huyu bwana (Mungu Amlaze mahala pema) Aliitumikia nchi kwa uzalendo wake wote ndio ukaona hata akateuliwa mara mbili kuwa Jaji, hizi habari maskini angepaswa kuziandika kuondoa mkanganganyiko kwa hawa wajinga
Sijui unamjuaje ila mimi navyomjua ni kwa namna nyingine usinilazimishe nikubaliane na mawazo yako mara nyingi mtu akifariki ni hekima ukanyamaza ukamwache apambane na mola kwani kwa imani zetu yeye ndiye anaona zaidi ya kile tunachokiona sisi
 
Ukiisoma mpaka katikati, unaishia hapo hapo. Maana sijaona nini hasa alichofanya Mzee Kwikima. Kwa sifa yake, Mwenyezi Mungu ni mtukufu mno. Hakuna kiumbe atakayeweza kumlaghai.

Tuombeane heri. Hizi nyingine ni zile sarakasi zetu tunazofanya chini ya jua, tukidhani tutamuweka sawa Mwenyezi Mungu. Tusimuhusishe na story, hasa zile zenye lengo la kuficha ukweli. Yeye ni kweli na atasima ukweli ulipo milele yote
Kwikima ndie alikuwa hakimu mkazi wa kwanza muafrika, kwikima ndie alikuwa kabidhi wasii wa kwanza muafrika lakini kama haitoshi ndie mtanganyika wa kwanza kupendekezwa na
Sijui unamjuaje ila mimi navyomjua ni kwa namna nyingine usinilazimishe nikubaliane na mawazo yako mara nyingi mtu akifariki ni hekima ukanyamaza ukamwache apambane na mola kwani kwa imani zetu yeye ndiye anaona zaidi ya kile tunachokiona sisi
Mimi kaka yangu mihayo (judge) alimlea kwenye taaluma ya sheria, lakini kwa ufupi kwikima alikuwa ni mtu wa carible yake ilikuwa ukimshuhudia mahakamani akiunguruma utafurahi, usichoke kujifunza lakini ukitaka kuujua unguli wa yule mnyamwezi funua judgements zake au kutana na mzee mihayo atakusimulia
 
Ukiisoma mpaka katikati, unaishia hapo hapo. Maana sijaona nini hasa alichofanya Mzee Kwikima. Kwa sifa yake, Mwenyezi Mungu ni mtukufu mno. Hakuna kiumbe atakayeweza kumlaghai.

Tuombeane heri. Hizi nyingine ni zile sarakasi zetu tunazofanya chini ya jua, tukidhani tutamuweka sawa Mwenyezi Mungu. Tusimuhusishe na story, hasa zile zenye lengo la kuficha ukweli. Yeye ni kweli na atasima ukweli ulipo milele yote
Kwikima amefanya mengi huenda wewe ulikuwa mtoto au hujazaliwa, hao ndio ma pioneer wa sheria ya Tanganyika, unaweza usimpite hata mtu mzima mmoja wa umri wa kuanzia miaka 60 katika fani ya sheria ashindwe kukueleza umaridadi wa kwikima, bwana mkapa alikuwa akimuita mnyamwezi mbishi.

Kwikima ndio hakimu mkazi wa kwanza mtanganyika, kwikima ndio kabidhi wasii wa kwanza mtanganyika, kwikima ndio pendekezo la kwanza la Philip Telford Georges (aliyekuwa Jaji mkuu baada ya uhuru akitokea visiwa vya Trinidad and Tobago) kwenda kwa mwl julius ili awe Jaji mkuu, itoshe tu kukwambia wapo wazee wengi walioifanyia hii nchi makubwa hutokuja kuwasikia, Mola Ampumzishe kwa Amani Advocate kwikima
 
Bwana Mohamed Said Waambie hawa mabwana wakafunue EAST AFRICA LAW REPORTS wazisome judgment za yule nguli wa sheria, inaonyesha ni watoto wa juzi
 
Back
Top Bottom