Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Fuatilia yatakayojiri kwenye mkutano wa Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, leo saa 4:00 asubuhi.
Mwabukusi anazunguzia suala la wamasai kuondolewa kwenye eneo lao kwa nguvu, na serikali imeondoa huduma zote za msingi kwao kama watanzania halali wa nchi hii. Kwa mujibu wa sheria, watu hawa wanapaswa kuondolewa kwa hiari baada ya kuridhiana namamlaka.
TLS inatoa rai kwa serikali kuonesha nia yake ya dhati kwa kurudisha huduma zote za kijamii kwa wananchi wa ngorongoro kwani ni haki yao ya msingi, pia viyuo vya kupigia kura virudishwe ili washiriki zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Baraza la uongozi TLS limeona sakata hili linahitaji ufuatiliaji wa kina, hivyo limeunda kamati maalumu ya kufuatilia kwa ukaribu, itaongozwa na Dky. Rugemeleza Nshala.
Aidha, TLS imeona tangazo la Waziri wa TAMISEMI kufuta vijiji vya Ngorongoro, na hakuna kifungu chochote cha Sheria kinachompa Waziri mamlaka ya kufuta vijiji. Waziri atoke asema sheria hiyo ilitungwa lini na wapi.
TLS itakaa tena kujadili pamoja na kukutana na Serikali kwa nia njema kuona namna ya kumaliza sintofahamu hii.
Kuhusu kadhia iliyotokea kwenye maadhimisho ya siku ya vijana iliyopaswa kufanyika Mbeya ambapo viongozi na wanachama wa CHADEMA walikamatwa na kuumizwa, Baraza la Uongozi wa TLS limeamua kuwafungulia mashtaka wahusika kutoka jeshi la Polisi kwa majina yao ili wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.