DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Akizungumza jijini Arusha hii leo Mei 8, 2025 katika mkutano wa TLS uliojadili hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, Mwabukusi amesema ni aibu kwa Bunge la Tanzania kushindwa kujadili masuala kama ukiukwaji wa haki za binadamu, usalama wa raia, vitendo vya utekaji na kupigwa kwa baadhi ya wananchi, pamoja na kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.
“Mambo haya yangepaswa kujadiliwa na bunge letu, lakini leo hii tunaona Bunge la Ulaya ndilo linayajadili. Hii ni ishara kuwa Bunge letu limekosa uthubutu na linaogopa wajibu wake,” alisema Mwabukusi.
Kauli hiyo imekuja saa chache baada ya Bunge la Ulaya kuketi na kuijadili Tanzania, likitoa wito kwa Serikali kuhakikisha haki inatendeka katika kesi ya Tundu Lissu, na kuweka mazingira rafiki kwa vyama vya siasa, hasa upinzani, kushiriki uchaguzi mkuu ujao kwa uhuru na haki.