Wakili Mwabukusi: Miezi 3 hakuna dalili Mahakama ya Rufaa kusikiliza Kesi ya Tundu Lissu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 11, 2026, amesema kile alichokiita "mbinu za makusudi" za upande wa mashtaka kuchelewesha shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Mwabukusi amebainisha kuwa tangu upande wa Jamhuri ulipopeleka maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa miezi mitatu iliyopita, shauri hilo limekwama huku kukiwa hakuna jitihada za kupanga jopo la majaji wa Mahakam ya Rufaa. Amesisitiza kuwa hali hii inasababisha mtuhumiwa kuendelea kusalia mahabusu kwa kosa ambalo halina dhamana, bila kesi yake kusonga mbele

"Mshtakiwa hajahusika hata kidogo na ucheleweshaji wa kesi hii. Mara zote tumemsikia akiomba kesi isikilizwe, hata wakati anapokuwa amenyimwa chakula, amenyimwa kuonana na mawakili wake, amekuwa akisisitiza kesi iendelee. Jambo ambalo tunakomendi (recommend) na ndio wito ambao mawakili tunasisitizwa mara zote kwamba tusiiahirishe mashauri bila sababu za msingi."

'
 
Samia ni Bata
 
Maelekezo ya samuya hayo, kwa akili yake anadhani hapo ndo kafunga kbs ukosoaji dhidi yake...kumbe ndo anazidisha chuki hajiulizi kwann hata akipost chochote mitandaoni anaambulia matusi!
 
Back
Top Bottom