Wakili Mwabukusi: Sioni kosa la Askofu Gwajima kukemea matukio ya utekaji nchini, hiyo ndio injili safi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika TLS Wakili Boniface Mwabukusi amesema waliofunga kanisa la Ufufuo na Uzima ndio wanahusika na utekaji.

Soma > Serikali yalifutia usajili Kanisa la Askofu Gwajima

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Juni 04, 2025 ofisini kwake jijini Mbeya.

Pia soma > Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!

Wakili Mwabukusi amesema haoni kosa la askofu Josephat Gwajima katika kukemea matukio ya utekaji nchini akisema hiyo ndio injili safi hivyo walioamuru kufuta usajili wa kanisa hilo ni watekaji au wanufaika wa utekaji kwa maslahi yao binafsi.

Pamoja na hayo, Rais huyo wa TLS ameeleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya Askari kutumia nguvu na kuwapiga wananchi waliokuwa mahakamani Juni 02, 2025 kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu bila kosa lolote.

Hata hivyo amewataka wahanga wa kupigwa mahakamani na kudhalilishwa wakafungue kesi Askari wanaohusika na vitendo hivyo kwa majina yao ili waweze kuliwalipa fidia.

Pia ameeleza suala la utekaji wa Mpaluka Said Nyagali (Mdude) kuwa bado wanaendelea na taratibu ili waliohusika na utekaji huo wawajibike ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Mdude anapatikana akiwa hai laasivyo haki yake itatafutwa ndani na nje ya nchi.

Katika mkutano wake huo na wanahabari, pia ameeleza kuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu (2025) TLS haifungamani na chama chochote cha siasa badala yake wanashauri kufanyika kwa uchaguzi wa huru, haki na usawa kwa wote na kwamba chama hicho kitatoa tamko hivi karibuni kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Injili safi au siyo? 👇👇
Screenshot_20250604-121227.jpg
 
Back
Top Bottom