Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani

Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.

Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?

kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?

Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"

Chanzo : Jambo Tv
Nilijuwa na nilisema kuwa kitendo cha Mwabukusi kuruhusu vyama vya siasa kudandia agenda yake ya DPW aliyoishaitengeneza vizuri ni kuiua agenda hiyo. Sasa yametia Mwarabu yuko Kurasini.

Hivi vyama kama vyenyewe havitaki kushirikiana vimeamua kuwa wateja wa CCM 5-1 unategemea unaweza kushirikiana navyo jambo ukalifanikisha kwa tija?

Bora Mwabukusi kama wao wapinzani ungechukuwa chako mapema.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni mchungu
Tulisema hakuna opposition Tz
Vyama vyote ni vikundi vya porojo
Kama opposition ipo maswala makuu muhimu wameshindwa kutafuta suluhu kutwa barabarani kama wakimbiza mwenge. Wanachowaza ni ‘siku tukichukua nchi wote watalipa gharama’ wanawaza uongozi tuuu.
Ukimya wao ni kuwapuuza wenye nchi ambao ni walipa kodi.
Cha kushangaza ni ukimya na kelele miiingi..
Ukimya upo kwenye:
Uuzwaji wa Bandari
Uuzwaji sijui iwekezaji KIA
Teuzi zisizo na msingi wala manufaa kwa Taifa

Mgomo baridi wa maandamano
Safari za mkulu
Ubadhirifu wa mali za Umma
Ufusadi uliopitiliza……

Kelele sasa miiiingi
Nyumba ya mwenyekiti
Utajiri wa Mwenyekiti
Endeleeni na join the nini sijui
Operesheni aka mbio za Mwenge
Wajinga ndio waliwao

Hii ni bs of the highest order!

Dr Slaa na mapungufu yake Taifa linamhitaji sana kuliko upinzani
Chadema wanatatuaje changamoto za Tanzania kwani wao ni serekali wanakusanya kodi
 
Najua mjadala nawe kwangu utakuwa mgumu sana, lakini ngoja nikuulize tu swali kuhusu haya uliyo andika hapa katika hiyo mistari miwili.
Hivi huo "ubovu wa sheria...) unao usema wewe, unaanzia wapi hasa mkuu 'Artifact'?
Hata hizo sheria nzuri zikiwepo, bila ya usimamizi mahsusi nyuma ya hizo sheria, unadhani hali itakuwa tofauti na ilivyo sasa?
Mimi ninakuomba tu uyatafakari haya ninayokuuliza, nina hakika jibu sahihi utalipata mwenyewe huko.
ccm wako bungeni asilimia 100 wabadilishe sheria mbovu ambazo haziwajibishi waizi wa mali za umma hio lawama tena unawapa chadema hii ni kali
 
Naamini Mbeya wanaweza kuanzisha chama cha ziada chenye mafanikio kwenye upinzani, isiwe kila muda vyama vyenye upinzani vianzishwe na watu wa Kilimanjaro (Ilianza Tlp, ikaja Nccr, sasa ni Chadema)
Umepotpsha tlp ni rwekwamwa, nccr ni mabere, cdm ni bob makani Kilimanjaro Iko wapi?? Una elimu ndogo na Chuki za ukabila,
 
Tusiteme big G kwa karanga za kuonjeshwa. Nadhani hujui motive ya Mwabukusi. Mwabukusi anatumia nguvu nyingi kuishambulia upinzani kuliko CCM. Kwanza kadai wapinzani wanafanya biashara ya demokrasia nk. Sasa kwa kauli Kama hiyo huyo yupo upinzani kwa lengo gani. Hapo kaipa CCM milage kubwa Sana.

Mimi simuamini Tena. Kuna kauli mtu akizisema unajua huyu sio mpinzani ana mission yake tofauti. Mtu unaushambulia upinzani kuliko hata Makonda na chongolo. Muangali Mwabukusi kwa jicho la mbali utaujua ukweli.
Nyie chadema si ndio mlijipendekeza kwake?acha awanyeee
 
Anasema ukweli, kuwa ni ukhanithi kwa wapinzani kuendelea kushiriki chaguzi hizi kwa mazingira haya ya kihanithi. Na hao wapinzani watakaokubali kushiriki huo uhuni uitwaa uchaguzi, watashangaa jinsi kutakakavyokua na wapiga kura wachache.

Wananchi wameshastuka hawana muda wa kufanywa mafala kwenye mstari wa kura, wakati ccm wamekuja na matokeo yao mfukoni. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataletaa mabadiko ya kweli kwenye chaguzi za nchi hii.


“Machafuko ama Mapinduzi ya kijeshi “

Bado sana JMT kufika huko.
 
Ni kweli anachosema Adv. Mwabukusi, siasa zetu kwa kiasi kikubwa zimegeuzwa kuwa ajira, na wala sio kuwatumikia wananchi kama walivyozoea kutudanganya.

Ndio maana unawaona wale wanawake 19 bado wako bungeni mpaka leo bila aibu yoyote, wanakula bure kodi za watanganyika, huku ajabu wakiwa bungeni nao wanajidai kulaani upotevu wa fedha serikalini, wao hawajioni!..

Huku wengine nao wameshasahau kama msimamo wa chama chao ni kutoshiriki uchaguzi, mpaka Katiba Mpya ipatikane, wao wameshaanza kusema watahakikisha wanawaondoa wabunge wa CCM majimboni mwao, hii kauli ni sawa na tusi kwa mtu mwenye spirit ya Adv. Mwabukusi.

Wapiga kura tunageuzwa mtaji wa wanasiasa bila kujua, sometime tuna siasa za kisanii sana, za kupitisha muda ili wale na familia zao, kwa wale walioupata utajiri kupitia siasa, kamwe hawawezi kuuacha uchaguzi upite mpaka waisubiri Katiba Mpya ipatikane.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Halafu kuna wapuuzi wanaamini kabisa kuwa mzee mbowe eti anajitolea kufanya siasa ,dah nchi hii ina wajinga aisee
 
wapi chadema imesema itashiriki uchaguzi? jiepushe na watu wa hovyo......usiwe kwenye kundi la mtu kutofungu post/thread yako akijua kuna rubbish!

Kuna namna ya kusema uliyonayo moyoni kwa wenzako ambao lengo lenu ni moja..... huyu kumbe mpuuzi tu.
Hivi kweli kuna wakumzuia lema kutokutafuta ajira ya pale Arusha eti kisingizio ni katiba mpya?
 
Halafu kuna wapuuzi wanaamini kabisa kuwa mzee mbowe eti anajitolea kufanya siasa ,dah nchi hii ina wajinga aisee
Kipindi billcanars inataifishwa, mashamba ya mbowe yanaharibiwa na kumbuka account za mbowe zimefungwa na zimefunguliwa wakati wa samia au kipindi hiko mbowe anafanyiwa hayo madhila ulikua bado mtoto
 
Mbowe anazingua, ila mwabukusi kuita wapinzani ni wabaya kuliko CCM Hilo ni tusi baya na dharau. Aanzishe chama chake Sasa.
Wachagga bana bado mnaamini kuwa chadema ni chama cha siasa?
 
Wachagga bana bado mnaamini kuwa chadema ni chama cha siasa?
Kipindi billcanars inataifishwa, mashamba ya mbowe yanaharibiwa na mkuu wa wilaya kule hai, na kumbuka account za mbowe zimefungwa na zimefunguliwa wakati wa samia au kipindi hiko mbowe anafanyiwa hayo madhila ulikua bado mtoto
 
Back
Top Bottom