carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Wakili Mwesigwa Siraji Mutabuzi, amemtaka Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili kuachia nafasi hiyo kama hawezi kusimamia misingi, taratibu na sheria zinazoongoza taasisi hiyo ya kitaaluma, badala ya kuanza kugeuza kuwa 'Jukwaa la Kisiasa'
Wakili huyo amedai kuwa, tangu Wakili Mwabukusi ashike nafasi ya kuongoza TLS amekuwa na mienendo isiyozingatia maadili na isiyokubalika kwenye uwanja wa sheria kwakuwa amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwasilisha au kufanya mambo ya kisiasa, kuanzia matamko yake na hata anavyoongoza, hivyo kumtaka kuacha tabia hiyo mara moja na kama inamuwia vigumu kuacha basi aachie ngazi ili wanachama wa TLS watafute Rais mwingine atakayewafaa
Amesema kwa muda mrefu, hata kabla hajawa Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi anafahamika mrengo wake wa kisiasa, na kipindi chote hicho amekuwa akifanya kazi zake za siasa, KUIKOSOA serikali na hata kuipeleka Mahakamani lakini hakuna aliyemnyooshea VIDOLE, lakini kwa sasa hawawezi kumvumilia kwakuwa anaongoza taasisi yao