Wakili Mwesiga Mutabazi amesema Mwabukusi aache TLS kwa kuwa sio chama cha siasa

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Wakili Mwesigwa Siraji Mutabuzi, amemtaka Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili kuachia nafasi hiyo kama hawezi kusimamia misingi, taratibu na sheria zinazoongoza taasisi hiyo ya kitaaluma, badala ya kuanza kugeuza kuwa 'Jukwaa la Kisiasa'

Wakili huyo amedai kuwa, tangu Wakili Mwabukusi ashike nafasi ya kuongoza TLS amekuwa na mienendo isiyozingatia maadili na isiyokubalika kwenye uwanja wa sheria kwakuwa amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwasilisha au kufanya mambo ya kisiasa, kuanzia matamko yake na hata anavyoongoza, hivyo kumtaka kuacha tabia hiyo mara moja na kama inamuwia vigumu kuacha basi aachie ngazi ili wanachama wa TLS watafute Rais mwingine atakayewafaa

Amesema kwa muda mrefu, hata kabla hajawa Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi anafahamika mrengo wake wa kisiasa, na kipindi chote hicho amekuwa akifanya kazi zake za siasa, KUIKOSOA serikali na hata kuipeleka Mahakamani lakini hakuna aliyemnyooshea VIDOLE, lakini kwa sasa hawawezi kumvumilia kwakuwa anaongoza taasisi yao



Your browser is not able to display this video.
 
Wakili Mwesiga yupo sahihi 100%

Naunga mkono hoja 🤝
 
Mutabazi who?
Anatokea wakili toka jalalani na kutuhumu misingi ya kuongoza TLS, ujue ametumwa au ni mtu wa Idara.
 
Angekuwa anasifia Mauaji ya Halaiki angekuwa sahihi siyo?
Mbona maneno ya Mwabukusi yanaeleweka?
Haki
Amani
Uwajibikaji
Nyie hataki Haki?
Nyie mnataka amani tu?
Nyie hamtaki wauaji wawajibike?
zingatia hoja na maelezo ya wakili Mwasiga bila kuleta porojo za kusadikika gentleman na itapendeza zaidi 🐒
 
Huyu Mwabukusi sijawi msikia akipigania lolote la kulinda maslahi ya TLS na mawakili Nchini. TLS na Mawakili halali wanakumbana na changamoto nyingi kuanzia kuzagaa Kwa mawakili feki (vishoka), mihuri ya mawakili feki, hata usalama wa mawakili kazini. Hayo maswali yote huwezi kuona tamko lolote kutoka Kwa Rais Mwabukusi.

Kama passion yake ni siasa, basi aingie kwenye siasa.
 
Subiri mwabukusi amalize muda wake ugombee ili ufanye hayo unayotaka TLS iwe..kelele za nini!
 
Unazijua kazi za rais WA TLS, lisu nimwanachama pia hapaswi kutetewa, au kizungumzia haki ni kosa kwa kiongozi anayesimamimia Taasisi ya kisheria
 
Nikiongea Mimi instinct desire naonekana nnachuki🤣

Taja kifungu cha sheria alichovunja Mwabukusi , maana TLS ni taasisi ya kisheria tunatarajia waseme kavunja kanuni ipi.

Hizi kelele ni sababu alikemea kuuzwa bandari na mbuga, kukemea utekaji na mauaji.

Si mara ya kwanza kulalamika akiwepo rais wa TLS mkosoaji kuanzia kwa Lissu na Fatma Karume mliongea ila Mwabukusi angekua anasifia hayo mambo msingemsumbua.
 
Kavunja Tanganyika law society act. 307
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…