Wakati Mwl. Julius K. Nyerere anaongoza mapambano ya kuwaondoa wakoloni nchini, lengo kuu lilikuwa Tanganyika ijitawale na haswa kutimiza ndoto yake ya kuliunganisha bara la Afrika kuwa kitu kimoja ili tuwe na nguvu kiuchumi na kiulinzi dhidi ya nchi za ulaya na kwingineko duniani.
Wakoloni hawakutaka kuachia nchi yetu kirahisi sababu ya mali ambazo walikuwa wakizivuna kutoka Afrika na hapa naizungumzia Tanzania.
Sasa mambo yasiwe mengi, mkoloni yule yule ambae uhusiano wake na nchi zetu za Kiafrika ni Uporaji-Rasilimali zetu haswa kwa ukoloni mamboleo uliopo hivi sasa, leo hii ndio eti ageuke kuwa mtetezi wa Rasilimali-Demokrasia na Rasilimali-Amani iliyopo Tanzania na Afrika?
Robert Amsterdam, hawezi kuwa wakili mkuu na mtetezi mkuu wa kiongozi mkuu wa Upinzani nchini kisha tukamuamini kuwa hana maslahi na ushindi wa kiongozi huyo katika madaraka ya Urais anayowania na chama cha CHADEMA.
Mzungu Bw. Robert Amsterdam hawezi kujivua ukoloni ulio ndani ya damu yake, hawezi kutetea maslahi halisi ya watanzania, kwa lipi? Kwa faida ya nani?
Lakini leo hii ndie wakili mkuu wa Lissu na wenzake wa CHADEMA, jinsi gani chama hiki kimechanganyikiwa.....ni sawasawa na mgombee mirathi ndani ya nyumba yenu kisha mmoja wenu asiye na akili akamuite jambazi wa kizungu aje kuiba za familia ilimradi watagawane nae chochote kitu.
Tamaa ya kutaka madaraka ya nchi isiwafanye viongozi wa upinzani kuvunja kuta za nyumba ili kuingiza wakoloni, vita hii tulishaimaliza kipinfi cha Mwl. Nyerere.