Pre GE2025 Wakili Nkuba linda heshima yako, msapoti wakili Mwabukusi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
GTs,

Ni heshima iliyoje kuona haki imetendeka na tena kwa uwazi kabisa kwa kijana Wakili Mwambukusi kuibuka mshindi.

Ni dhahiri Wakili Nkuba hakuwa kabisa na uwezekano wa kushinda. Najua michezo yetu wana CCM ya kupenyezana kila sehemu ila hapa tukubali tumeshindwa na ndiyo maana nakuomba Wakili Nkuba achana na kwenda mahakamani kupinga ushindi halali wa Wakili Mwambukusi.

Kumbuka hao hao Mawakili ndiyo watu wako na ndiyo utakaofanya nao kazi maisha yako yote. Haikusaidii kabisa kupinga kile ambacho Mungu kaamua, na elewa hali ya sasa watu wengi hawaipendi CCM kwa sababu na wizi, rushwa, ufisadi, na uzembe.

Kwa maantiki hiyo hata vyombo vya ulinzi na usalama haviwezi kupinga maamuzi ya wengi na ndiyo maana hata CCM 2025 inaweza kushindwa mchana kweupe akipatikana mgombea mbadala mwenye ushawishi maana wananchi wamechoka mno kusikia kila siku report za CAG na hazifanyiwi kazi.
Mwenzako anasikiliza maagizo ya Chama
 
Kumbuka hao hao Mawakili ndiyo watu wako na ndiyo utakaofanya nao kazi maisha yako yote. Haikusaidii kabisa kupinga kile ambacho Mungu kaamua, na elewa hali ya sasa watu wengi hawaipendi CCM kwa sababu na wizi, rushwa, ufisadi, na uzembe.
Sikuweza kujizuia kuyanyanyua haya maneno uliyo andika hapo kabla ya kusoma hadi huko mwisho wa bandiko lako.

Watu wa aina yako wapo wengi sana ndani ya CCM na nje ya chama hicho. Laiti kama wengi wenu mngetambua umuhimu wa maamuzi yenu juu ya taifa letu hili, sina shaka hali yetu ingekuwa na matumaini mazuri.
Ni bahati mbaya sana kwamba maamuzi yenu ni mpaka maslahi binafsi yaingiliwe, hapo ndipo mnazinduka na kukumbuka umuhimu wa Tanzania yetu hii.

Hata hivyo, nikupongeze sana, kwa sababu sijawahi kukusoma popote humu JF kwa aina ya mawazo kama ulivyo yawasilisha hapa, tena kwa ufafanuzi wa kina kabisa; mbali ya vile vi-mistari viwili, vitatu, kila mara kuisifia CCM.
Sote, kwa nyakati tofauti, tumewahi kuwa karibu na hiki chama cha CCM; lakini kimebadilika sana, na tukaamua kubaki na Tanzania tu basi. Siku moja mkiinyosha CCM, nani ajuae, tunaweza kuwaunga mkono tena.
 
Haya pia twayatalajia hapo baadae kwenye chaguzi zetu zijazo
Iwapo Samia atakuwa ndiye mtu wa kuwaamsha watu akili namna hii, nami kwa hakika nitamsifu sana huyu mama 'Chura Kiziwi' kwa kazi yake nzuri hii. Shukrani zangu nyingi zitatimia kwake kama chaguzi za Serikali za mitaa na ule mkuu 2025 utaendeshwa katika mazingira kama haya yaliyoonekana TLS. Sitakuwa na lawama juu ya matokeo hao, hata kama CCM watakuwa ndio washindi wa chaguzi hizo.
 
Id imekuwa hacked. Hii id haina akili hii.
Nimejaribu kukutafuta sana mkuu, Tindo' baada ya kuyaona haya yanayo tokea sasa. Kwa bahati nzuri, kumbe tupo sote hapa!

Sina shaka unakumbuka sababu inayonifanya nikukumbuke, kila mara mambo ya aina hii yanapojitokeza, hata kama ni katika ngazi hii ndogo ya TLS.
Wewe unakumbuka, ile nadharia yetu muhimu tunayo ijadili mara zote na kutofikia maafikiano kila mara.
Kumbe "Kususia kupiga kura" siyo njia pekee iliyo baki kuwaonyesha CCM kuwa hawatakiwi tena.

Nategemea, baada ya kushuhudia haya yaliyo tokea kwa Mwabukusi, kwamba wewe na mimi tutashirikiana kuwahimiza waTanzania wajitokeze kwa wingi kabisa nyakati za chaguzi zinazofuata kupiga kura zao kwa viongozi wanao wataka wenyewe. Kazi ya kuhakikisha kura zao hazivurugwi na yeyote, wawasikilize vyama vya upinzani mipango itakayo elezwa kuzuia uhalifu huo uliozoeleka kwa CCM.
Matumaini yangu ni kwamba, sote sasa, wewe na mimi, tutakuwa ukurasa mmoja katika swala hili.
 
Iwapo Samia atakuwa ndiye mtu wa kuwaamsha watu akili namna hii, nami kwa hakika nitamsifu sana huyu mama 'Chura Kiziwi' kwa kazi yake nzuri hii. Shukrani zangu nyingi zitatimia kwake kama chaguzi za Serikali za mitaa na ule mkuu 2025 utaendeshwa katika mazingira kama haya yaliyoonekana TLS. Sitakuwa na lawama juu ya matokeo hao, hata kama CCM watakuwa ndio washindi wa chaguzi hizo.
🙏🙏🙏
 
Nimejaribu kukutafuta sana mkuu, Tindo' baada ya kuyaona haya yanayo tokea sasa. Kwa bahati nzuri, kumbe tupo sote hapa!

Sina shaka unakumbuka sababu inayonifanya nikukumbuke, kila mara mambo ya aina hii yanapojitokeza, hata kama ni katika ngazi hii ndogo ya TLS.
Wewe unakumbuka, ile nadharia yetu muhimu tunayo ijadili mara zote na kutofikia maafikiano kila mara.
Kumbe "Kususia kupiga kura" siyo njia pekee iliyo baki kuwaonyesha CCM kuwa hawatakiwi tena.

Nategemea, baada ya kushuhudia haya yaliyo tokea kwa Mwabukusi, kwamba wewe na mimi tutashirikiana kuwahimiza waTanzania wajitokeze kwa wingi kabisa nyakati za chaguzi zinazofuata kupiga kura zao kwa viongozi wanao wataka wenyewe. Kazi ya kuhakikisha kura zao hazivurugwi na yeyote, wawasikilize vyama vya upinzani mipango itakayo elezwa kuzuia uhalifu huo uliozoeleka kwa CCM.
Matumaini yangu ni kwamba, sote sasa, wewe na mimi, tutakuwa ukurasa mmoja katika swala hili.
Sibadilikibadiliki, hakuna tume huru ya kweli ya uchaguzi siwezi ama hata kushawishi watu wajitokeze kupiga kura. Bado naamini machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio njio za kweli za kuwatoa hawa majizi. Ww endelea kushawishi uwezavyo, na mimi naendelea vizuri kuhakikisha watu wengi hawajitoezi kushiriki hayo maigizo yaitwayo uchaguzi.
 
Umeliweka vizuri hili sasa. Kwa upande wangu, anagalau naanza kuwa na matumaini kutokana na haya tuliyo yashuhudia ya TLS, na nina hakika mfano huu utakuwa chachu ya matumaini zaidi kwenda mbele kama wapinzani (soma CHADEMA), watajuwa namna ya kuelezea mfano huu vizuri kwa wananchi tokea sasa hadi chaguzi ziishe.
Nazidi kuimarika katika imani kwamba haitakuwa lazima kwa Tanzania kuingia kwenye "machafuko, au mapinduzi" ili kuwaondoa CCM madarakani. Hii kazi inazidi kuonekana kuwa inawezekana sana.
 
Sipingi unachoamini, bali siamini unachoamini.
 
Back
Top Bottom