Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Omari Hamisi Omari, ameeleza kuwa kisheria mume au mke hana haki ya kushika au kupekua simu au vifaa vya mawasiliano vya mwenza wake bila ridhaa. Amefafanua kuwa Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda haki ya faragha ya kila mtu katika familia na ndoa, jambo linalompa kila mwanandoa uhuru kamili wa faragha kwenye vyombo vyake vya mawasiliano.
Aidha, Wakili Omari ameongeza kuwa Vifungu vya 56 na 58 vya Sheria ya Ndoa vinaimarisha ulinzi huo kwa kubainisha wazi kuwa mke na mume wana haki ya kumiliki mali zao binafsi kama vile simu walizozinunua wao wenyewe, jambo linalowanyima haki wanandoa kuingiliana katika mali na vifaa vyao binafsi.
Ameonya kuwa kupeleleza simu za wanandoa wenzao kupitia mtandao na teknolojia, akisisitiza kuwa chini ya Kifungu cha 6 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act) inayohusu uingiliaji haramu wa mawasiliano (illegal interception), ni kosa kubwa la kisheria linaloweza kusababisha adhabu kali ikiwemo faini ya hadi shilingi milioni tano za Kitanzania.