Wakili Pasco Mayalla -A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part II

Wakili Pasco Mayalla -A True Story of My Life: Nilitamani kuwa Wakili sababu ya Wakili Murtaza Lakha, sasa ni Wakili. Je, nitakuwa kama Lakha? Part II

Mkuu why usilikwapue?
Mkuu Duduvwili, ili mtu uweze kukwapua kitu chochote, lazima kwanza uwe na kitu kinachoitwa "mens rea" ya ukwapuaji, ndipo uweze kufanya "actus reus" (kitendo) cha ukwapuaji!, it's very unfortunately, mimi sio mkwapuaji!.
nimependa sana mtiririko mzima wa masimulizi jambo jingine ningependa kufahamu hatma ya Mzee Mayalla je itaelezwa kwenye sehemu ya Mwisho?
Asante, subiria last part.
P
 
✓Kaka Pascal hbri,nimepitia historia ya maisha yako nikagundua kuwa:we Ni mpambanaji Sana na kamwe hukati tamaaa Hadi upate like unachokitaka!!!
✓Nakuomba kitu kimoja ya kwamba Kama itawezekana andikia kitabu historia ya maisha yako itakuwa chachu Sana kwa watanzania na watu duniani kwa ujumla kutimiza ndoto zao
 
It's true, japo nilisoma LL.B UDSM kwa 4 years, from 2003 nikahitimu 2007, LL.B yangu nimekuja kukabidhiwa 2017!. Ten years after graduating!.

Wakati nikiwa mwaka wa 4, matokeo ya mwisho, nika clear. Jina langu nikaliona kwenye list ya graduation. Hivyo nikajihesabu ni graduant.

By then, part of family inaishi nje ya nchi, hivyo nikatimka zangu to join the family for a family matters.

Kumbe huku nyuma kuna mwalimu alifuta matokeo yangu ya somo lake ambalo nilikuwa nimepata A, kwa hoja kuwa mimi ni mtu anayenifahamu, hakuwahi kuniona hata mara moja kwenye somo lake!.

Hivyo jina langu likaondolewa kutoka graduation list na mimi
nikapigwa a technical disco kwa kufutiwa matokeo mengine yote as an absentee without mimi knowing maana siko nchini.

Niliporudi nchini 2008, nikaanza kushughulikia clearance yangu, baada ya kukamilisha kila kitu, kufika hatua ya mwisho, wakati wanataka ku print cheti changu ndipo wakukuta jina limekatwa, hivyo halipo kwenye graduation list!.

Ndipo nikaanza ku trace back to back ndipo nikakuta matokeo yangu ya mwisho yamefutwa yote!.

Ku trace reasons ndipo nikaikuta hiyo hoja kuwa somo hilo nililopata A, sikuwahi kuhudhuria hata kipindi kimoja!. Mwalimu ananijua in person, hivyo hajawahi kuniona!.

Ukiwa maarufu, a local TV personality kwa kujulikana kwa sura ni shidah!. Ili uwe free kwenye mambo fulani you have to disguise and be incognito, somo lake kila siku, nilikuwepo, signing sheet nasaini, ila nilikuwa nakaa back bench, incognito nimepiga kapelo na sun gogle's, siulizi swali lolote wala sichangii hoja yoyote, teacher akawa anadhani sipo!.

Records za attendence register zipo zikaonyesha nilikuwepo, Mwalimu aliyefuta matokeo yangu, aliyafuta kinyume cha sheria, kama ni kweli hajaniona kwenye kipindi chake, alipaswa aniripoti ili nizuiwe kufanya UE, kama course work zote nimefanya, jina lipo kwenye attendance register, mtihani wa EU nimefanya, na nikapata A, hakuna sheria ya kumfutia mwanafunzi matokeo eti kwasababu unamjua ni maarufu na hujawahi kumuona kwenye kipindi chako!.

Utambulisho wa mwanafunzi kuhudhuria kipindi ni attendance register na sio Sura!.
Justifications ya kufanya EU, ni attendance register na kukamilisha course work, na sio mwalimu kukujua sura!.
Wakati namaliza UDSM, Dean alikuwa ni Dr. Ibrahim Juma.

Wakati nahangaikia cha kufanya ndipo nikala ule mziga wa bike Pascal Mayalla apata ajali.....
Sikuweza tena kushughulikia.
Mwaka ukapita
2009 nikawa fit kuanza shughuli mdogo mdogo na nilishuka humu JF kushukuru Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
usumbufu ulipozidi nikaachana na kufuatilia, nikaenda zangu UK, kufanya Kazi FCO, nikapangiwa BHC DAR.

Ndipo nikarudi UDSM kumaliza mambo yangu, nikakuta Dean ni Prof. Sifuni Mchome, nikakubaliwa nitapewa cheti changu cha kuhitimu LL.B ila sasa sheria imebadilika nitatakiwa kwenda law school!.

It took me almost 10 good years to be recognised as a bonafide LL.B holder in 2017 baada ya jina langu kuingizwa upya Kwa graduation ya 2018 watu wakadhani ndio nime graduate!.

Baada ya ku graduate 2007 jina kuingizwa 2018, it took 5 more years kupata uwakili, 2022!. Kiukweli hii safari ya uwakili wangu ni ndefu, yenye milima na mabonde, vidimbwi, madibwi, mito na vijito na sasa ndio hatimaye nimeifikia bahari, jee nitavuka?.
P
utavuka mkwe wangu Mungu yupo
 
✓Kaka Pascal hbri,nimepitia historia ya maisha yako nikagundua kuwa:we Ni mpambanaji Sana na kamwe hukati tamaaa Hadi upate like unachokitaka!!!
✓Nakuomba kitu kimoja ya kwamba Kama itawezekana andikia kitabu historia ya maisha yako itakuwa chachu Sana kwa watanzania na watu duniani kwa ujumla kutimiza ndoto zao
Hao Watanzania wanasoma vitabu? Nyumbani kwako kama kuna wadogokozi pesa hifadhi kwenye kurasa za vitabu zitakaa salama kabisa hakuna mtu atagusa.
 
Duh...!, Mkuu Matola, Mimi na Abou ni ndugu wa damu tumesoma nae darasa moja, chuo kimoja TSJ, tukilala chumba kimoja. Tukaomba kazi pamoja sehemu moja na kuajiriwa siku moja position moja pale RTD, ofisi ikatupangia nyumba moja, Flat pale Ilala Sharif Shamba tukaanza maisha pamoja. Tulikuja kutengana baada ya wote kuoa nyumba ikawa ndogo.

Msiba kwa Abou ni msiba wangu, naamini unajua ni msiba wa nani na uhusiano wa msiba huo na wazee wa Kaunda Suti!.

Pale ni nyumbani kwa Abou, Mimi kwa upande wangu, wazazi wangu wote wawili walikuwa wàtumishi waaminifu na maofisa waandamizi wa Idara, na ni kweli Idara huwa wana recruit from within ila sisi tumezaliwa watoto 8, hivyo hata kama Idara wana recruit watoto wa wana Idara, we can't all 8 of us be recruited huko!. Ndugu zangu 6 wako serikalini, wawili ndio tuko sekta binafsi. Siwezi kujua kuhusu ndugu zangu ila mimi sio!.

Mtu wa Idara, hawezi kuleta humu issues kama hizi, TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Au hii Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Ningekuwa ni mtu wa kule issue kama hii ingetua mezani kwa DGIS na yeye aipeleke kwa CinC, lakini mimi niliileta humu, na hao jamaa wakaipuuzia mwisho wa siku, jamaa wakala kichwa!.

Au nilipotoa angalizo hili, US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? ningekuwa mimi ni mtu wa kule, hoja hizi si ningeziwasilisha kule, zikafanyiwa kazi!. Matokeo yake hoja hizi zilipuuzwa mwisho wa siku tukalizwa!.
P
Ni mda sasa ila basi tu
 
Back
Top Bottom