PostGE2025 Wakili Peter Madeleka amshtaki Rais Samia kwa kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9

PostGE2025 Wakili Peter Madeleka amshtaki Rais Samia kwa kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika, Desemba 9

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Joined
May 4, 2024
Posts
37
Reaction score
190
Wakili Peter Madeleka amshtaki rais Samia kwa kufuta sherehe za Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, (Desemba 9) katika Mahakama ya Tanzania Masjala Kuu ya Dodoma.

Soma: Sherehe za sikukuu ya Uhuru zapigwa STOP. Fedha kutumika kurekebisha miundombinu iliyoharibika wakati wa Uchaguzi Mkuu

1764076619485.png

Screenshot 2025-11-25 162130.png
 
Anapenda sherehe yule mtu wa tabora
 
Hivi Sherehe lazima ziendani na matumizi ya pesa ?!!!!

Nashauri Sherehe hawa jamaa tunaowalipa mapesa yetu mengi na hakuna value for money (maisha kitaa yanazidi kuwa magumu na hakuna sera za kueleweka) waliojipeleka Bungeni tuwapatie Mifagio na mafyekeo waingia kitaa na kutufanyia Usafi...
 
Nchi yoyote inayojitambua lazima iadhimishe Uhuru wake kwa shughuli rasmi ya kiserikali na siyo lazima yatumike mabilioni ya pesa. Ukiona watawala wanaondoa sherehe za uhuru ni kwamba wanataka kuwaondolea uhuru wenu.

Rais anaweza kwenda pale UDSM akaongelea topic ya "Uhuru wa Mtanzania". Mwaka mwingine, Rais anaweza kukutana na asasi za kiraia akatoa hotuba kuhusu haki na wajibu wa raia. Mwaka mwingine akatembemea kambi ya jeshi akakagua gwaride na kuongelea hali ya usalama wa nchi na kushukuru juhudi na mchango ya vyombo vya Ulinzi katika kulinda mipaka ya nchi. Haya mambo yote hayahitaji pesa yoyote kuyatekeleza lakini yanakumbusha umuhimu wa Uhuru.

Pitia uzi nilioleta jana kuhusu suala hili.

 
Huyu jamaa anapenda attention, kesi zake nyingi zinaishia njiani isitoshe alisaliti no reform no election mnafiki mkubwa.
 
Wakili Peter Madeleka amshtaki rais Samia kwa kufuta sherehe za Maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, (Desemba 9) katika Mahakama ya Tanzania Masjala Kuu ya Dodoma.

Soma: PostGE2025 - Sherehe za sikukuu ya Uhuru zapigwa STOP. Fedha kutumika kurekebisha miundombinu iliyoharibika wakati wa Uchaguzi Mkuu


View attachment 3507383
Huyu nae mimi huwa simuelewi katiba tuliyonayo mbovu na rais hashitakiwi kipindi kama hiki angekuwa bize huko kwenye mahakama za kimataifa hata hapo maakama ya east africa tu ila wapi yeye anataka kupambana na katiba ambayo teyari haiwezi kutoa haki kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom