Wakili Robert Amsterdam ni nani?

Subirini kupanga foleni ya kuwapelekea ugali hao wenzenu pale ICC
Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee the name says it all.
 
Pia msifikiri tumesahau kuwa jao mnaodai kuwa walisaini mikataba hotelini ndio 2015/walikuwa wagombea urais ws CHADEMA. Hivyo CHADEMA ilishapiteza credibility kutoka 2015
 
Mtaweweseka mwwka huu. Lissi kawatafutia mwarobaini. Na sasa hivi pona yenu ni kuacha kuiba kura kama kushinda mshinde kwa haki( ambapo hamwesi kushinda kwa hakika) la sivyo mtakutana na Mkono wa Amsterdam. Jamaa anashinda kesi kwa Putin na venezuela kwenye udikitet uliokomaa hapa kwa uchwara itakuwaje?
Anyway nimemskikia Mahera anatetemeka ati kamtumia barua ya kumtisha.
 
Bora hata huyo anaweza akawa aliwatetea Acacia.. Ila Deo Mwanyika aliyelipishwa ambillion na Magufuli nae rafiki damu damu wa Magu mpaka kazawadiwa fursa ya kugombea ubunge kupitia chama cha Magufuli.. CCM kama CCM halisi isingeweza mpa nafasi fisadi aliyethibitishwa kama Deo Mwanyika fursa ya uongozi ndani ya chama na jaribio la kumuingiza Bungeni.
 
Mbona Kabudi mwanasheria nguli Waziri wa mambo ya nje katulia tuli kuhusu jambo hili? Hakika anajua tabu iliyopo mbele anawaachia mazuzu muingie haswa Jiwe
 
 
WEWE JITU LA UTUMWA WA FIKRA. IT SEEMS TO YOU AS LONG AS UTUMWA ANAUENDESHA MWAFRIKA SIYO HOJA, AKIWA MZUGU NDIYO INAKUWA HOJA? RUBBISH
 
Mataga huna akili.

Haki za binadamu hujaziona hapo!?
Yani unamtetea Putin thidi ya Kodokhovsky.
Jinga sana
 


Mtetezi wa majambazi!!!,hapo ndipo CCM mnapokosea
Macho yanaona namna haki inavokandamizwa na utawala wenu dhalimu kuwahi kutokea katika awamu zote nchi hii,people die like FLIES every day
Watu wanapewa makesi ya ajabu ajabu eti ikionekana tu una vision au mission tofauti na serikali hii

Ukombozi wa MWENYEZIMUNGU unakuja taratibu na uzuri hata ule mtaji wenu wa wajinga kule vijijini taratibu unaanza kutoweka

Mkubali ninyi ni WAKOSEFU na muanze kujirekebisha hapo, KIBURI ndicho kilichowaangusha MADHALIMU wote duniani
 
Mabeberu yakiamua mbuzi jike lazima atazaa tu
 
Reactions: Ole
Amani bila HAKI hilo halipo ni mwendawazimu tu ndio anaweza akaamini hivyo.
 
Kuna msemo wa Mwanafilosofia Plato unaosema, ‘’An empty vessel makes the loudest sound, so they that have the least wit are the greatest babblers.”

Wahenga wetu pia walisema, ‘’debe tupu haliachi kuvuma.

Mwanasheria huyu wa Tundu Lissu anaonekana kama mtangazaji wa siasa za Tanzania badala ya mwanasheria.

Wanasheria mahili nchini kama Peter Kibatala huwezi kuwaona wanasema sema ovyo au wanapiga kelele bali kazi zao ndio zinawasemea.

Huyu Mwanasheria wa Lissu unakuta anauliza maswali halafu anajijibu mwenyewe! Kibaya zaidi, anaaminisha baadhi ya watu wajinga kama ndiye ‘’masiha’’ wa Tundu Lissu kuingia Ikulu au eti Rais Magufuli kushitakiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu!

Ukimchunguza kwa undani utagundua bado ana fikra kuwa akiwatisha viongozi nchini au kusema sana basi watafanya anachokitaka. Kinachofurahisha zaidi, hao anaowapigia kelele au kuwatisha inaonekana wamempuuza! Yeye anapiga kelele, wao wanatenda ‘’by hook or by crook’’!

Kibaya zaidi, huyu mwanasheria hawajui Watanzania vizuri! Kwa watanzania hawa, huu uchaguzi kwao ni ‘’bygone’’. Hakuna maandamano wala vurugu za kisiasa kama anategemea zitatokea ili iwe ‘’chachu’’ ya kuingilia masuala ya kisiasa nchini!

Huu Uchaguzi Mkuu tumeshuhudia wanasiasa wa Marekani wakitoa matamko mengi kuzidi hata baadhi ya ahadi wagombea Urais nchini!

Kuna dhana inajengwa eti kuwa Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi. Hakuna cha vikwavyo vya kiuchumi bali kilichoko ni ‘’competing economic interest and benefit’’ kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kimataifa hasa Marekani na Kanada. Kelele za baadhi ya wanasiasa wa Marekani ni baada ya Symbion Power Tanzania Ltd (SPTL) kupigwa ‘’kufuli’’ na serikali. Serikali ilikuwa inalipa zaidi ya Tsh bilioni 700 kwa mwaka kwa haya makampuni (Symbion, IPTL na Aggreko).

Tanzania kama nchi ingewekewa vikwazo vya kiuchumi kama tungekuwa tumewafukuza wawekezaji wa nje kama alivyofanya Rais Robert Mugabe. Yaani utawekewaje vikwazo wakati makampuni makubwa ya kimataifa ya uwindaji, gesi na madini bado yanaendelea kuvuna faida nchini huku yakisafirisha madini kwenye masoko ya nchi zinazodaiwa zitaweka vikwazo.

Hata ‘’Targeted individual sanctions’’ kwa wanasiasa wa Tanzania ni kupoteza muda tu kwa sababu wanasiasa wenyewe hata kusafiri nje ya nchi hawasafiri na pia hawana hata ‘’big asset’’ kwenye nchi inayosemekana itaweka vikwazo! Ndiyo yaleyale ya Makonda kuwekewa vikwazo huku akiendelea kudunda mitaani!

Baada ya muda, huyu ‘’mwanasheria wa Tundu Lissu’’ atapotea kwenye siasa za Tanzania kimya kimya na kumuacha Tundu Lissu abebe mzigo wake baada ya misheni ya kuingia Ikulu ‘’kugonga mwamba’’!

Namfanisha Tundu Lissu na mwanasiasa wa Venezuela, Juan Guaido ambaye alitumiwa sana na wanasiasa wa Marekani ili kumuondoa Rais Nicolas Maduro wakitegemea ana uwezo na nguvu za kisiasa kwa wananchi wengi lakini baadaye ikagundulika hana uwezo au nguvu hizo.

Wanasiasa wa Marekani baada ya kugundua hana uwezo na nguvu za kisiasa wakaachana naye. Wabunge wa kambi ya upinzani pia wakamuondoa kwenye kiti cha kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

Tundu Lissu naye ataachwa kimya kimya kama ilivyotokea kwa Juan Guaido kwa sababau wanasiasa wa Marekani na Kanada hawana urafiki wa kudumu bali wana maslahi/manufaa ya kudumu.

Tundu Lissu ameshindwa kuleta maslahi/manufaa ya kudumu kwa wafanyabiashara wa Marekani na Kanada ambapo malipo yake ni kumuacha aubebe mzigo wake mwenyewe kama walivyofanya kwa Juan Guaido!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…