mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,369
- 5,866
Kama umenielewa hutapata tabu kuona kuwa huyo wakili anachokifanya sio sahihi, kinachoonekana ni vitisho na kuingilia michakato ya Taasisi za Taifa huru,
Huwezi mwambia mkuu wa Taasisi flani kuwa usipofanya hivi kwa mteja wangu nitahakikisha unapelekwa ICC au kuwekewa vikwazo.
Kila mchakato unataratibu zake za kuukabili na taratibu hizo hazifanani, Pili barua zake hazina madhara kisheria kwa hapa nyumbani kwani hana kibali cha kufanya shughuli za uwakili ni za kupuuzwa tu, tatu kesi za Uchaguzi huwa hazipelekwi ICC, kule zinakwenda kesi za jinai zinazohusiana na mauaji ya kimbari, maswala ya uchaguzi yanashughulikiwa na mifumo iliyowekwa ndani ya nchi husika.
Kuhusiana na maswala ya vikwazo lazima kuwe na maazimio ya nchi wanachama wa jumuiya za kimataifa ukiachana na vile vikwazo vya nchi moja moja. I.e US ama EU kwa Sasa dunia haiendeshwi na tena na kauli za Taifa moja maendeleo yametapakaa kona ya dunia hivyo ukikosa hapa unapata kule, hakuna tena monopoly katika upatikanaji wa vitu, hivyo mikwara haifui Sana dafu .
Tanzania tumekuwa na chaguzi za amani na hakujawahi tokea matukio ya kupelekea mtu kuhitajika ICC au kuwepo vikwazo vya kimataifa, hatuna historia hiyo wala kwa Sasa hakuna viashiria vya hayo kutokea, amani imetawala na uchaguzi utapita JPM na Mwinyi wakikamata usukani na sisi tukiendelea kulijenga taifa letu pendwa Tanzania.
jambo muhimu ni kwa viongozi waliozoea kufungia raia ndani na kutesa kutambua sasa dunia ni kijiji. Zama za kutesa watu kama mifugo yao imepita.Madikteta hawako salama