myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
Asante sana mkuu....nimekuelewa sana.Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.Anyway,
Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"
Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.
Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.
=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):
Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.
Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"
Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"
Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.
Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).
The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.
Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.