carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Aliyekuwa Meya wa Kampala Erias Lukwago, ambaye pia ni wakili wa kiongozi wa upinzani Dr. Kizza Besigye, ameripotiwa kukimbizwa Hospitalini kwa matibabu ya dharura baada ya kupata matatizo makali ya kiafya akiwa mahabusu.
Taarifa zilizotolewa na naibu wake wa zamani Doreen Nyanjura Omutatina zinasema Lukwago alipokelewa katika hospitali ya Kitaifa ya Mulago kutokana na shida za kupumua na matatizo ya uti wa mgongo yanayohusiana na upasuaji wa awali.
Lukwago amekuwa akipambana na maumivu ya muda mrefu ya mgongo na alishauriwa kufanyiwa uchunguzi zaidi nje ya nchi, lakini hali yake imezidi kuwa mbaya akiwa kizuizini.
Tukio hili linajiri wakati Lukwago anakabiliwa na mashtaka ya misprision of treason, akidaiwa kushindwa kuripoti njama zinazohusiana na Besigye.
Madaktari wa Mulago wanatarajiwa kufanya uchunguzi zaidi huku wafuasi wake wakisubiri taarifa rasmi kuhusu hali yake.
Chanzo: Mwanzo tv plus