PostGE2025 Wakili wa haki za binadamu: Watuhumiwa maandamano Dar hakuna raia wa kigeni

PostGE2025 Wakili wa haki za binadamu: Watuhumiwa maandamano Dar hakuna raia wa kigeni

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakili na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Maduhu William amesema kuwa hadi sasa hakuna ushahidi unaoonesha kuwapo kwa mtuhumiwa yeyote ambaye si raia wa Tanzania miongoni mwa mamia ya vijana waliokamatwa kutokana na maandamano na vurugu zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

1764060329046.png

Akizungumza na The Chanzo, Wakili Maduhu amesema timu yao imefanya uchunguzi wa kina katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam, ikiwemo Gereza la Segerea na vituo vya polisi, na kubaini kuwa watuhumiwa wote waliowahoji ni Watanzania.

Wakili Maduhu amesema kuwa katika Gereza la Segerea, LHRC ilipata nafasi ya kuwauliza moja kwa moja watuhumiwa 300 kama miongoni mwao kulikuwa na mtu asiye raia wa Tanzania. Aidha, Maduhu ameeleza kuwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, ambako LHRC inawasimamia watuhumiwa saba, hakuna hata mmoja ambaye ni mgeni.

“sasa allegations au tuhuma za kwamba kuna watu waliandamana au lugha ambao wanatumia 'walifanya fujo kutoka mataifa mengine ya nje', mimi binafsi kama wakili sitaki sana kuzungumzia kwa sababu zilisemwa na mamlaka zingine, nafikiri watu wenye uwezo wa kuzungumza kama kulikuwa na waandamanaji au watu wa kutoka mataifa mengine ni hao waliozileta hizo hoja”, ameeleza.

Wakili Maduhu amesema kuwa hata katika hatua za kusikiliza mashauri mahakamani, LHRC imekuwa ikiomba majina ya watuhumiwa yasomwe kwa uwazi ili kubaini utambulisho wao. Hata hivyo, Wakili Maduhu amebainisha kuwa taarifa zao zinahusu Dar es Salaam pekee, kwani mikoa mingine inaendeshwa na mawakili walio katika maeneo hayo.

Kauli ya Maduhu imekuja siku chache baada ya baadhi ya viongozi wa serikali kudai kuwa sehemu ya vijana waliokamatwa kutokana na vurugu hizo walikuwa ni raia kutoka mataifa ya kigeni.
 
Back
Top Bottom