Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 3,499
- 5,956
Wakili wa Kimataifa, "Robert Amsterdam" amerusha mawe mawili gizani kwa kuisakama na kuiponda serikali ya CCM inayoongozwa na Raisi Samia Suluhu Hassan kwa ukandamizaji wa haki, sheria na uonevu kwa Raia wa Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa X Robert Amsterdam ametweet na kusema, "Tunampongeza @TunduALissu kwa jitihada zake za kujitetea binafsi, kwani ni wazi kuwa amenyimwa kwa njia isiyo halali haki ya kupata huduma ya kisheria kwa usiri na kwa mujibu wa sheria kutoka kwa wenzetu waliopo Tanzania. Tutaendelea kupigania haki yake, na haki za Watanzania, katika jukwaa la kimataifa." (Tarehe 16-June-25, 1:15 PM)

Leo tarehe, (17-June-2025), Robert Amsterdam ametweet tena na kusema, "Serikali ya Tanzania inajaribu kuficha ukweli, si tu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, bali pia kutoka kwa wananchi wake."
Huku akisisitiza kuwa juhudi zake katika uwanja wa kimataifa zitaendelea kama kawaida mpaka haki ya Raia Watanzania na Tundu Lissu zipatikane.
Tutaendelea kusimama pamoja na @TunduALissu — si kwa sababu ya jina lake, bali kwa sababu anawakilisha sauti ya Watanzania wanaodai uwajibikaji, sheria, na demokrasia ya kweli.
#Haki #Sheria #TumeUhuru #KatibaMpya #Tanganyika